Serikali, wabunge na suala la mikopo ya wanafunzi hamlifahamu

mwamola

Senior Member
Joined
May 28, 2012
Posts
109
Reaction score
15
Kwanza nianze kuomba radhi kama sijaielewa sana hoja ya Mh Nchemba ya mfuko wa Elimu ya juu. Nasema naomba radhi kwa sababu kama serikali muda wote imekuwa ikijisifia kwa kuongeza fedha ktk kufanikisha wote walio na sifa ya kupata mkopo wa Elimu ya juu wanapata, iweje leo hii tuanzishe tena kitu ambacho naweza kukiona kama ni parallel to HESLB?Pili, Nadhani serikali na wabunge mnatuchezea tu. Nasema mnatuchezea kwa mambo yafuatayo; a) Pale Bodi ya Elimu ya juu maafsa mikopo wale sidhani kama wanafahamu wajibu wao na hata sijui kama nyie wabunge na serikali mnatambua majibu na aina ya huduma watoazo wale maafsa pale bodi ya mikopo.Nimesema maafsa hawatambui kazi ni ipi kwa sababu ukifika kwa huduma hizo utasikia mwingine anakwambia kwanza kwa nini unafuatilia mkopo wakati tayari muhula unakaribia kwisha kwani si ujilipie tu? Kibaya nikiwa hapo ndani alikuja bwana mmoja nadhani anasoma shahada ya uzamili ama uzamivu.
Alipoeleza kuwa nae hajapata mkopo tena hafahamu sababu zilizomsababisha asipate mkopo alijibiwa na nyie si mjisomeshe tu yaani wewe unasoma shahada ya Uzamivu unafuatilia mkopo? Kajisomesheni kwa mishahara yenu. Baya zaidi pia ni kuwa pale ndani kila mtu nadhani ni kama kachanganyikiwa vile. Nasema hivyo kwa sababu yule dada alimjibu hivyo yule bwana aliekuwa anafuatilia mkopo na akamsisitizia kuwa wale wa Uzamivu wote wameshapewa mkopo. Lakini mie nina ndugu yangu anasoma UZAMIVU hajapata mkopo huo. Nasema serikali na wabunge tatizo la mikopo hamlifahamu ya nini kuanzisha Mfuko wa elimu wakati wahudumu ndo wanatoa majibu kama haya?
 
inayoshughulikia mambo hayo si inafahamika? Acheni hizo au kwakuwa waajiriwa wengi ni watoto wa wakurugenzi wa mashirika mbalimbali ya umma ndo mnadhani hata watoto wa wakulima wanaweza kujilipia ada na gharama zingine? Nenda ofisi namba 24 ukasikie majibu yao na hata kule mbele zaidi ya namba hii yaani thelath
 
Nenda namba thelathin kuna yule mdada anayekaa karibu na yule jamaa usikie vimbwanga, kuna siku nlipandwa na hasira nkataka kumtia makofi ila jamaa mmoja wa ofisi nyingine namba 27 akaniita na kunambia niachane nae eti ana stroke, wanakera balaa
 
Namba 24 kuna dada mnene hivi yuko very kind and polite! Pia ni hardworker
 
Sema taratibu mkuu! Naumia sana kwani nimeandika barua kufanya special exams kwa sababu ya heslb kutoniletea pesa tikea mwaka wa masomo 2012/2013 ianze,kwani tuition fee yangu wala meal and accomodation bado,alafu wanataka nifaulu vizuri na kufanya project yangu hii vizuri.......mungu anajua
 
It pains alot,hata mimi bodi hawajaleta pesa yangu toka oktoba(SUA),na hakuna updates zzte toka bodi na tar11 2naanza ue.Heslb is no longer credible,ni maharamia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…