Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema wamepokea malalamiko kwamba kuna Shule zinazuia Wanafunzi kwenda likizo bila kushauriana na Wazazi huku Wazazi wengine wakitakiwa kulipa ili kuwaweka Wanafunzi Shuleni ambapo amewataka Viongozi wa Shule kutambua kuwa ni haki ya Mwanafunzi kwenda likizo.
Akiongea Jijini Dodoma Mkenda amesema “Kwa Shule za Serikali kuna mwongozo umetolewa na Kamishna wa Elimu wa siku za kufunga na kufungua Shule, ni muhimu sana tukajifunza kuzingatia huo mwongozo ili Wanafunzi wapate muda pia wa kupumzika, nahimiza Wakuu wa Shule wote na Wakurugenzi wazingatie utaratibu huo"
"Kwa Shule binafsi Kamishna alisema waangalie kalenda lakini wanaweza kufanya adjustment kulingana na mahitaji yao lakini ukweli unabaki palepale kwamba Wanafunzi wetu wanahitaji kupumzika"
"Wito wetu ni kwamba tusipelekee Kamishna atoe waraka wenye masharti makali kwa Shule binafsi, Wanafunzi wana haki ya kupumzika, likizo zimewekwa ili Watoto wapate muda wa kupumzika, wakae na Wazazi wao, wapate kucheza vilevile na kubadilisha mazingira na hii huwa inawasadia"
Soma mijadala ya kulalamikia wanafunzi kubaki shuleni: