Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Katika juhudi za kupambana na maambukizi ya #Corona, Serikali kupitia Wizara ya Afya imetaka Masoko, Magulio na Minada kuhakikisha inazingatia umbali kati ya mtu na mtu, na kila mwenye biashara kuweka vifaa vya kunawia mikono.
Aidha watu wasio na kazi maalumu wametakiwa kutoonekana kwenye masoko ili kuepusha misongamano isiyo ya lazima.
Pamoja na hayo, Wizara imezuia mambo ya kuwawekesha watu kama kuchoma nyama ili watu wanunue nyama na kwenda nayo nyumbani badala ya kusubiria na kusabbisha msongamano.