Kuna tatizo mahala, nadhani kuna wajanja wanamdanganya Samia waendelee kutupiga watanzania, haiwezekani tozo mpya kila kukicha mpaka wanasahau kama walishatudanganya sababu ya tozo hizo, barabara tozo, huku kuna mkopo toka bank ya dunia kwa ajili ya barabara.
Huyu Rais wetu aamke, aiangalie serikali yake anayoiongoza inaendaje, ni kama vile amekaimu majukumu yake kwa wasaidizi wake kwa kujua, au bila kujua, ni vurugu.
Nimeona kwenye gazeti tozo kwenye vituo vya mafuta, reli, saloon, nk hizi pesa zote zinaenda wapi? mwananchi mmoja mwenye saluni yake akatwe tozo kwenye saluni, bei ya mafuta, miamala ya simu, na kodi ya majengo kwa luku, huu ni ujinga, sio ubunifu.
Tuliambiwa Magufuli alikuwa anawaibia watu pesa zao akajenge miundombinu, sasa iweje pesa alizoiba Magufuli zitoshe kuendeleza hiyo SGR na Nyerere Dam wakati hii serikali ya Samia inahangaika kubuni kila aina ya tozo? hapa tatizo ni vichwa vya hawa viongozi, sioni sababu nyingine.
Pamoja na yote haya bado utasikia uhaba wa vyumba vya madarasa, na ukosefu wa maji safi na salama.
Samia aamke toka usingizini, haya mambo amewaachia wengine wayafanye badala yake yataendelea kumsababishia achukiwe na wananchi, na kudharauliwa, aanze kuwa mfuatiliaji yeye binafsi, asikae tu ofisini na kupanda ndege kila siku.