Serikali wekeni tozo kwenye vifaa vya upako

The seer

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
407
Reaction score
690
SERIKALI WEKENI TOZO KWENYE VIFAA VYA UPAKO

Napenda kuishauri serikali kupitia mamlaka ya mapato tanzania kuweka tozo kwenye biashara ya vifaa vya upako inayofanyika kwenye makanisa baadhi ya kilokole,siku za karibuni kumezuka biashara yenye kuingiza mabilioni ya pesa inayofanywa na baadhi ya watumishi wa makanisa ya kilokole

Biashara hii huhusishwa uuzaji wa

1. Maji ya upako. Azam pamoja na kulipa kodi anauza lita kwa kiasi cha Tsh 1000,lakini hawa wajasiliamali kanisa huuza kwa kiasi cha 2000 mpaka 5000 bila kodi, napendekeza serikali ichukue tsh 700 kwa lita na nabii abaki na kiasi kinachobaki.

2. Keki ya upako. Baadhi ya makanisa kipande cha keki ni tsh 10,000 napendekeza tozo iwe tsh 35,00 kwa kipande

3. Kisima cha upako. Kuvuka kisima cha upako zoto iwe tsh 2000 kwa kichwa.

4. Leso ya upako, bei ni kati ya tsh 2000 mpaka 5000 tozo iwe tsh 700

5. Kumuona nabii, baadhi ya manabii hucharge kiasi cha Tsh 20,000 mpaka laki mbili ili kuonana na nabii, serikali iweke tozo ya Tsh 12,000.

6. Tango la upako, iwe zero tozo.

NB. Biashara hii imewapatia mabilioni ya pesa baadhi ya manabii ambao wanaishi maisha ya kifahali tofauti na waumini wao ambao wengi wanaishi kwenye umasikini mkubwa,na ujinga mkubwa ambao wengi hudangwanya kuwa maisha mazuri watayakuta mbinguni.

Ukisoma maandiko biashara hizi zilikwepo tangu kipindi cha Yesu, ambapo ukisoma marko 11 mstari wa 15 na kuendelea Yesu aliingia hekaluni na kupindua meza na kufukuza wafanyabiashara hekaluni na kuwaambia imeandikwa nyumba yangu itatwa nyumba ya sala na si pango la wanyang'anyi.

N.B UJINGA WA WAUMINI KUTOKUJUA MAANDIKO UMEKUWA MTAJI WA MANABII. WA UONGO KUJIPATIA UTAJIRI.
 
Title: Maisha ya Marekani ukimya upweke magari
content inazungumzia Tozo
mzee hii mixing ya double kick,jobo, na mmea bila shaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…