Lamwike JF
Huku kijijini kwetu Njelela kilichopo Kata ya Mundindi, Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe kuna Mwalimu anatutesa sana, kwa sasa amekaimu Utendaji wa Kijiji baada ya Mtendaji aliyekuwepo kwenda likizo ya uzazi.
Mwalimu huyo (jina nalihifadhi kwa muda) anachotutendea sisi Wakazi wa Njelela ni unyanyasaji na ukatili, kwanza akikuhisi umetenda kosa bila kutafuta ushahidi, bila kukuuliza anakuita na kukuadhibu.
Adhabu hiyo ni kukuchapa fimbo haijalishi wewe ni mtu mzima au kijana, anatandika kama anapiga nyoka.
Hivi karibuni alimchapa mtu mmoja baada ya kumkuta na kosa analolijua yeye. Baada ya kumchapa akampa faini ya shilingi laki tatu ikiwa atashindwa basi watauza nyumba yake akamwambia na mteja ameshapatikana.
Cha kusikitisha nyumba ile wameshaiuza na kijana wa watu hana pa kuishi tunajiuliza hizo pesa walizouza nyumba (milioni 6) ziko wapi?
Kubwa kuliko amempiga kijana mwingine juzi tu hadi akamvunja mguu wa kulia, tulipofika Hospitali ya Lugarawa wakasema hadi PF 3, Tulivyoenda Polisi wakamhitaji mtu aliyefanya unyama huo.
Mwalimu akaitwa alipofika akaomba jambo hilo limalizwe pembeni lisiende Mahakamani kwamba atagharamia matibabu ya mtu huyo.
Sasa sisi Wananjelela tutateswa na huyu mwalimu hadi lini? Kwakuwa yeye ana pesa kidogo anaona fahari kutufanyia ukatili. Anatubambikia kesi kwa makosa yasiyoeleweka akikuhisi tu kwa lolote. Unaadhibiwa. Sasa hivi amani imetoweka vijana na wazee wote tumejawa na uoga wa kufanyiwa lolote na mwalimu huyu.
Sio Afisa Elimu aliyechukua hatua dhidi yake wala Mtendaji wa Kijiji, anafikiri tumesahau? Au kwakuwa yeye ni Mtumishi wa Serikali anajiona yuko juu ya Sheria kwa kufanya chochote atakacho?
Kupitia jukwaa hili tunaomba hatua zichukuliwe, tunataka amani ya kijiji chetu irudi hatutaki kuishi kwa hofu ya kumwogopa mtu. Tunataka tunywe ulanzi na ughimbi kwa amani ile tuliyoizoea.
Ujumbe huu umfikie Mkuu wa Wilaya, tunaomba sisi wananjelela tusikilizwe na tupewe haki yetu ya kusikilizwa endapo kuna makosa yametokea na sio kuadhibiwa kama watoto wadogo.
Nidaliha🙏