Serikali Wilayani Misungwi izuie uonevu kwenye hospitali ya Misasi

Serikali Wilayani Misungwi izuie uonevu kwenye hospitali ya Misasi

Samiaagain2025

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2020
Posts
3,626
Reaction score
3,869
Wakuu habarini,

Kuna vituko sana hii nchi mpaka unaweza kuchanganyikiwa.

Katika hospitali ya MISASI iliyoko wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza.

Kuna tabia ya waganga/wauguzi kuwaambia wagonjwa wanunue baadhi ya vifaa rahisi sana vinavyotakiwa kuwa hospitali.

Na vilevile walipie pesa kwa waganga/wahudumu hao kama fadhila kwa kazi yao.

Mfano mtu anaambiwa anunue gloves na sindano ambavyo ni lazima vipatikane hospitali.

Tunaomba serikali izuie huu uonevu maana tunaamini ni kinyume na sera za wizara ya afya na maadili kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom