Serikali ya Chad yakaidi wito wa wananchi na upinzani wa kufuta na kurudia upya Uchaguzi!

Serikali ya Chad yakaidi wito wa wananchi na upinzani wa kufuta na kurudia upya Uchaguzi!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Hali ya mvutano inaendelea nchini Chad baada ya vyama vya upinzani kutaka kumalizika kwa haraka kwa serikali ya mpito nchini humo na kufutwa kwa uchaguzi mkuu uliofanyika Desemba 29.

Kwa mujibu wa upinzani, uchaguzi huo ulisusiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi na hivyo haupaswi kuendelea

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Chad (ANGE) imeahidi kuendelea na mchakato wa kuhesabu kura na kutangaza matokeo rasmi.

Makamu wa Rais wa ANGE, Assane Bairra, amesema kuwa licha ya changamoto zilizojitokeza, uchaguzi huo ulikuwa wa haki na uwazi. Kwa mujibu wa tume hiyo, asilimia 36 ya wapiga kura waliosajiliwa walishiriki katika uchaguzi wa mitaa, majimbo, na bunge.

“Tume yetu imehitimisha kipindi cha mpito kwa kuandaa uchaguzi wa kidemokrasia,” amesema Bairra. Matokeo ya awali yanatarajiwa kutangazwa ifikapo Januari 15, 2024.

Hata hivyo, vyama vya upinzani vimepinga takwimu hizi, vikidai kuwa asilimia 90 ya raia walijibu wito wa kususia uchaguzi huo.

chad elections.png

Msemaji wa Kundi la Wanasiasa wa Chad (GCAP), Avocksouma Djona, amesema kuwa wananchi wamechoshwa na utawala wa muda mrefu wa Mahamat Idriss Deby, ambaye alirithi uongozi baada ya kifo cha baba yake, Rais Idriss Deby Itno


Kabla ya uchaguzi huo, vyama vya upinzani vilimtuhumu Deby kwa kupanga kuiba kura, madai ambayo serikali imeyakanusha. Mchambuzi wa kisiasa kutoka Chuo Kikuu cha N’djamena, Yamingue Betinbaye, amesema madai ya upinzani yana mashiko, akionyesha wasiwasi kuhusu uwezekano wa masanduku ya kura kujaa kura feki zinazomfaa Deby.

==================================================================

An uneasy calm hangs over Chad, where the opposition is calling for an immediate end to the country’s transitional government and the cancellation of the December 29 general elections, which the opposition says were highly boycotted.

Chad's elections management body has pledged to count the votes and declare the results, saying irregularities cannot influence the outcome.

Assane Bairra, vice president of Chad's National Agency for the Management of Elections (ANGE), said vote counting is under way after the central African state’s local, provincial and parliamentary elections on Sunday.

The elections were scheduled to end Chad's three-year transition period following the death of longtime President Idriss Deby Itno in April 2021.

Source: The Citizen Digital
 
Back
Top Bottom