Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 44
Serikali yetu ni inashangaza. Jana TBC1 imeripoti kuwa mkuu wa wilaya huko Kilombero anasimamia mchakato wa kutaka kuhamisha wanakijji wa kijiji cha Namawala huko Kilombero kinyume na matakwa yao ili mwekazaji apewe ardhi ya kijiji kulima miwa.
Yaani Wanakijiji watanzania wanaokaa katika kijiji kisheria wahamishwe kutoka kwenye ardhi yao yenye rutuba apewe Mnyonyaji. Hii tabia ya serikali inayoota mizizi inatofautiana vipi na wakoloni ambao walichukua ardhi yetu yenye utajiri wa maliasili? Hivi wanakijiji ndio wanaostahili kukaa maeneo yasiyofaa? Tumesikia huko Loliondo sasa wanaelekea Kilombero, hii ni serikali gani isiyojali wananchi wake kwa kiwango hiki? Hivi serikali inaajenda ya siri ya kurudisha ukoloni nchini kwetu? Wananchi wanataabika tayari kwa hali ngumu ya maisha, serikali ikiendekeza sera ya kunyanganya ardhi watanzania ambayo ndiyo tegemeo lao na kuwapa wanyonyaji hali itakuwaje?