Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,962
- 721
Nimekutana na hii story kwenye Tanzania Daima, nimebaki nashangaa. Ni lini serikali yetu ilifanya research na ku-come with this finding. Soma mwenyewe.
Mkuchika akataza simu shuleni
na Halfani Lihundi, Arusha
SERIKALI imepiga marufuku matumizi ya simu za mikononi kwa wanafunzi wa shule za sekondari wawapo shuleni, kwa maelezo kuwa simu hizo zinasababisha wanafunzi kutokufanya vizuri katika masomo yao.
Kwamba simu hizo pia husababisha tamaa na vishawishi kwa wanafunzi kwani baadhi yao hulazimika kutafuta fedha za kununulia muda wa maongezi hata ikiwalazimu kufanya matendo maovu.
Amri hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kapteni mstaafu, George Mkuchika, wakati akifungua mkutano wa walimu wakuu kutoka mikoa yote nchini na nchi za jirani.
Mkutano huo, una lengo la kujadili changamoto zinazokabili sekta ya elimu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na maandalizi ya Tanzania katika kukabili changamoto hizo.
Mkuchika alisema mwanafunzi anapojiunga shuleni kwa mara ya kwanza huwa zinachukuliwa taarifa zote za mzazi au mlezi ikiwemo namba za simu ili kuwasiliana naye panapotokea matatizo na kwamba hata mwanafunzi wa kutwa anaporudi nyumbani kila siku anaweza kueleza matatizo yako, hivyo hakuna sababu ya wao kuwa na simu wakiwa shuleni.
Mkuchika alisema wizara yake ndiyo yenye mamlaka na maamuzi ya mwisho juu ya shule za sekondari, hivyo imezitaka bodi za shule kuandaa kanuni zitakazowabana wazazi na wanafunzi katika matumizi ya simu kwa wanafunzi na wizara itasimamia ili kuakikisha kuwa mkakati huo unafanikiwa.
Akisoma risala ya wakuu hao wa shule za sekondari, Mwenyekiti wa Taifa wa umoja wao (Tahosa), Bonus Ndimbo alibainisha changamoto zinazowakabili na kusababisha kazi yao kuwa ngumu.