Serikali ya Jubilee ilikopa na kutumia zaidi ya $4B bila ridhaa ya bunge, umuhimu wa katiba mpya ni upi?

Serikali ya Jubilee ilikopa na kutumia zaidi ya $4B bila ridhaa ya bunge, umuhimu wa katiba mpya ni upi?

Katiba mpya sio jibu la matatizo yanayoikumba nchi yetu, hili nitalisema kila mara na sitoogopa kutukanwa.

Suluhisho la matatizo yetu kama taifa ni kuwa na viongozi wenye utayari wa kuheshimu sheria zetu na misingi ya utawala bora.

Tanzania, kuanzia Rais hadi wenyeviti wa serikali za mitaa, hakuna mwenye utayari wa kuziheshimu sheria zetu. Wako tayari kufuata zile zinazowapendeza tu.

Hatuna haja ya katiba mpya,tuna haja ya kubadilisha mitazamo ya viongozi wetu. Waache kujiona 'mababa' na wajione kuwa ni viongozi waliowekwa kwa mujibu wa sheria na wanapaswa kuzifuata sheria.
 
Back
Top Bottom