SI KWELI Serikali ya Kenya imeingia makubaliano na serikali ya Ujerumani kuruhusu Wakenya 250,000 kwenda kufanya kazi Ujerumani

SI KWELI Serikali ya Kenya imeingia makubaliano na serikali ya Ujerumani kuruhusu Wakenya 250,000 kwenda kufanya kazi Ujerumani

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Naomba msaada kujua uhalisia wa swala hili upoje juu ya makubaliano yaliyosainiwa kati ya serikali ya Kenya na Ujerumani kubadilishana wafanyakazi 250,000 kutoka Kenya.

photo_2024-09-16_12-41-27.jpg
 
Tunachokijua
Vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii iliripoti kuwa Kenya wamesaini mkataba wa ushirikiano na ujerumani mkataba ambao unatoa nafasi kwa wakenya kwenda kujifunza nchini Ujerumani na wakenya wenye taaluma na ujuzi mbalimbali watakwenda kufanya kazi nchini Ujerumani.

Mkataba huo ulisainiwa Berlin, Ujerumani mbele ya kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais wa Kenya William Ruto 13 september, 2024.

Mkataba huo umesainiwa mara baada ya kupitia vipindi viwili vya majadiliano ya makubaliano kati ya nchi hizo ambayo yalifanyika Nairobi na Berlin mwaka huu 2024. Kwa mujibu wa Shirika la kazi duniani ILO wameeleza kuwa makubaliano ya kwanza yalifanyika February, 2024 Berlin na awamu ya pili yalifanyika tarehe 14&15 Mei, 2024.

Baada ya mkataba huo taarifa mbalimbali zilisambaa na kuleta sintofahamu kwa kueleza kuwa kupitia mkataba huo wakenya laki mbili na elfu hamsini (250,000) wenye ujuzi na taaluma mbalimbali watapata fursa hizo za kwenda kufanya kazi nchini Ujerumani ikiwemo shirika la utangazaji la Uingereza BBC kupitia taarifa waliyoichapisha tarehe 14 Septemba, 2024, wengine ni hapa .

Ukweli upoje Kuhusu idadi ya wakenya watakaopata nafasi hizo?
JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kubaini Rais wa Kenya William Ruto kupitia taarifa kwa vyombo vya habari aliyoitoa 5 Mei, 2023 jijini Nairobi akiwa na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Ruto alielezea kuwa mbali na mambo mengine waliyojadili na Kansela huyo, wamekubaliana pia kuhusu nafasi za kazi 250,000 kwa wakenya wenye ujuzi na taaluma mbalimbali nchini ujerumani ili kuendana na uhitaji mkubwa wa wafanyakazi nchini Ujerumani.

JamiiCheck imepitia taarifa mbalimbali ikiwemo iliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani kuhusu mkataba huo ambao hawajaeleza ni watu wangapi wenye ujuzi watapata nafasi ya kufanya kazi nchini Ujerumani, taarifa iliyotolewa na ikulu ya Kenya kupitia mtandao wa X pia hawajaeleza ni wakenya wangapi watapata nafasi hizo, lakini pia taarifa aliyoichapisha Rais Ruto kupitia mtandao wake wa X haijaeleza pia idadi kamili ya wakenya watakaopata nafasi hiyo.

Lakini pia wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani imekanusha taarifa ya BBC iiyotaja idadi ya wakenya watakaopata nafasi nchini Ujerumani kupitia Mtandao wa X na kusema kuwa taarifa hiyo ni uongo kwani hakuna sehemu ya makubaliano hayo ambayo inaonesha idadi au kiwango cha Wakenya wenye ujuzi watakaopata nafasi ya kufanya kazi Ujerumani na badala yake waombaji wote watatakiwa kufuata vigezo vilivyopo kwenye sheria ya wahamiaji wenye ujuzi ya nchini Ujerumani.

photo_2024-09-16_12-41-27-jpg.3097357

Aidha Shirika la utangazaji la Uingereza BBC wamefuta taarifa yao ya awali katika mtandao wa X na kupitia makala yao waliyoichapisha katika tovuti yao tarehe 15, Septemba, 2024 wameweka masahihisho kuhusu taarifa yao ya awali waliyoitoa tarehe 14 Septemba, 2024 iliyoweka idadi ya wakenya wenye ujuzi watakaopata nafasi ya kwenda kufanya kazi nchini Ujerumani kutokana na mkataba huo na kueleza kuwa wamefanya masahahisho ya taarifa hiyo baada ya kusahihishwa na Wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani kwamba mkataba huo hauna sehemu iliyotaja idadi kamili ya wakenya wenye ujuzi watakaopata nafasi.

1726497408355-png.3097581
Back
Top Bottom