Serikali ya Kenya kuondoa vikosi vyake Somalia

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Kenya ina mpango wa kuondoa vikosi vyake vilivyopo nchini Somalia ifikapo mwaka 2021, ili kuepuka mashambulio ya kigaidi yanayoendelea nchini humo.

Wizaya ya ulinzi ya Kenya kupitia kwa Waziri wa wizara hiyo Balozi Monica Juma, hivi karibuni itaanza mazungumzo kuona namna ya kurejesha vikosi vyake kutoka nchini Somalia, vikosi vilivyopelekwa kwa lengo la kuimarisha ulinzi nchini humo.

Vikosi vya Kenya viliingia rasmi nchini Somalia mwaka 2011 ili kuvisaidia vikosi vya nchi hiyo kukabiliana na wanamgambo wa Al Shabaab ambao wamekua wakifanya mashambulio katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na katika nchi jirani ya Kenya.

Kuendelea kwa mashambulio hayo ya Al Shabaab nchini Kenya kumechangia kupunguza idadi ya watalii wanaoitembelea nchi hiyo, kwa kuwa wengi wao wamekua wakihofia usalama wao.
 
Walichelewa sana! Kwa maana hiyo wame surrender to the mujahideen Alshabaab?

The winners are the terrorists, they've killed many Innocents in Kenya but Kenyans bragged on not surrendering, at last they've agreed to leave Mogadishu!

So bad, lost lives and resources for conducting military operations have perished as disposed!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usalama kwanza popote pale watalii wamepungua kwanini wasiondoe majeshi yao mwaka huu ili kuanza kukuza kukuza uchumi kwa sekta ya utalii mapema!?
 
Jisomee taarifa wewe mwenyewe, usikubali kupotoshwa. >>>Kenya to start talks on KDF exit from Somalia Vikosi vyote vya Umoja wa Afrika(AU) chini ya mission ya AMISOM vinaondoka Somalia mwaka wa 2021. Hiyo ilikuwepo kwa calender tangu hapo awali. Sio kwasababu ya mashambulizi ya kigaidi au vitu kama hivyo. Mashambulizi ya kigaidi hayajaongezeka, yamefifia na kikundi haramu cha alshabaab kipo kwenye pumzi zake za mwisho. Ifikapo 2021 mafunzo ya kijeshi ya vikosi vya Somalia na polisi pia yatakuwa yameisha na wataweza kudumisha amani wao wenyewe.
 
Usalama kwanza popote pale watalii wamepungua kwanini wasiondoe majeshi yao mwaka huu ili kuanza kukuza kukuza uchumi kwa sekta ya utalii mapema!?
Kando na masuala ya kiusalama, kiutalii au kiuchumi Kenya imefanikiwa kupambana na alshabaab na kuwezesha na kuimarisha serikali ya Somalia bila kusahau azma na strategy ya 2011 ya kutengeneza jamhuri mpya ya Azaaniya(Jubaland) ndani ya Somalia kama bufferzone ya nchi ya Kenya. Ndio maana Ethiopia walianza kuruka ruka walipostukia kwamba Kenya imefanikiwa hadi ikamueka rais Sheikh Madobe madarakani. Sasa hivi hamna cha Somalia, nchi hiyo imegawanyika kwenye vipande vipande. Somaliland, Puntland na Jubaland hadi hivi majuzi wameanza kupigana wenyewe kwa wenyewe. Baada ya vikosi vya kijeshi vya 'serikali kuu', Somalia, kushambulia vikosi vya Jubaland.
 
makafir huaga mna viherehere sana ila kwa mujahideena mtatosha tu kenge nyie
 
TUNAWASHUKURU SANA VIONGOZI WETU HAPA TZ. WALIONA MBAAAAAALI TOKEA MWANZO. HAWAKUTAKA KUJIINGIZA NA KUTAFUTA UHASAMA NA WATU. MATOKEO YAKE NI KUDUMU KWA AMANI IMARA NCHINI. POLE KWA WAKENYA KWA KUCHELEWA KUGUNDUA WALIPOKOSEA.
 
Kiherehere chao mbele ya Marekani, shobo ziliwaponza , uwezo mdogo Wanakimilia vita, matokeo yake Raia wasio na hatia wanaangamia.
TUNAWASHUKURU SANA VIONGOZI WETU HAPA TZ. WALIONA MBAAAAAALI TOKEA MWANZO. HAWAKUTAKA KUJIINGIZA NA KUTAFUTA UHASAMA NA WATU. MATOKEO YAKE NI KUDUMU KWA AMANI IMARA NCHINI. POLE KWA WAKENYA KWA KUCHELEWA KUGUNDUA WALIPOKOSEA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
What has KDF got to show us in all 10 years of War against the Militia Al Shabaab.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lesson, Never pick unnecessary fights in life.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiherehere chao mbele ya Marekani, shobo ziliwaponza , uwezo mdogo Wanakimilia vita, matokeo yake Raia wasio na hatia wanaangamia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kuwa Mjinga nani kama hatunge peleka soldiers wetu huko,hawa watu wangeingia kenya na wakishachukuwa Kenya next ni Tanzania na Uganda,Acha kuwa mjinga,na wakichukua Kenya Hakuna East africa,in short East na Central Africa itakuwa useless coz kila country itakuwa unstable so hakuna growth going on
 
Wacha uongo, mashambulizi ndio yameongezeka sana Al-Shabaab launches record 16 raids in Kenya within two months

Kwa kifupi Kenya wameshindwa kufikia malengo yake ktk hii vita, Lengo kuu lilikua ni kuzuia Alshabaab kuvuka mpaka na kuishambulia Kenya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii dhambi itawafuata wakenya siku zote kumbe nyinyi mlienda kwa dhumuni la kuigawanya Somalia Mungu anawaona
 
Alshabaab hawana lengo la kuchukua nchi yoyote ile zaidi ya kuweka utawala wa kiislamu ndani ya Somalia, ninyi mlijipeleka wenyewe kwa ujinga wenu. sasa vita imewasinda na mumepata hasara kubwa na wakenya wengi wameuliwa ndio mnafikiria kuondoka Somalia, hovyo kabisa ninyi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii dhambi itawafuata wakenya siku zote kumbe nyinyi mlienda kwa dhumuni la kuigawanya Somalia Mungu anawaona
Wao ndio wana dhambi, Jubaland ni bufferzone ya nchi ya Kenya kila nchi inaangalia maslahi yake. Hivi unajua kwa mwaka mmoja Kenya huwa inatumia hela ngapi kwasababu ya wakimbizi wa kisomali ndani na nje ya kambi kama Daadab? Ongezeka juu yake presha kwenye vitu kama miundo mbinu mashule na hospitali na uhalifu pia.
Lesson, Never pick unnecessary fights in life.
Sasa ni nani aliyechokoza mwingine kati ya Kenya na magaidi? Au hujui kwanini KDF wapo Somalia?
What has KDF got to show us in all 10 years of War against the Militia Al Shabaab.
Amani Kismayu ambapo meli zilikuwa zinatekwa kila uchao baharini. Jamhuri mpya ya Jubaland, n.k, n.k.
 
Analysis yako ni ya kiboya kupindukia. Mashambulizi 16 tena madogo madogo ya kuvizia kwenye boda utayalinganishaje na mashambuli mengi makubwa tena ndani kabisa ya Kenya kabla na KDF ilipoingia Somalia? Hao magaidi walituchokoza wenyewe kwa kuhuhujumu uchumi wa Kenya baada ya kuingia hadi pwani ya Kenya na kuteka watalii. Meli ambazo walikuwa wanateka baharini zilikuwa zinatukosti sote hapa Afrika Mashariki. Sasa hivi Kismayu ndio mji wenye amani zaidi ya zote Somalia. Alafu kule Mogadishu kwenye vita sio jurisdiction ya KDF.
 
Unaongelea nini mzee?
Hakuna unalojua wewe, Huna uelewa wa Kujadili na mimi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
You will try to go around as usual but the underlying truth behind the truth is the War is there for the interests of the Might US and his allies, nyie huko mlienda sababu ya kitu kidogo na kuuza mkaa in return of lives of hundreds of inocent Kenyans.
Unajua kwenye Maisha hata usipofanikiwa kuwa na pesa, ukijitambua tu wewe mshukuru Mungu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…