Ikaria
Member
- Jul 17, 2019
- 93
- 238
Siku chache tu baada ya Rais William Ruto kulishtumu Shirika la Ford Foundation kutoka Marekani kwa kile alichokitaja kama 'kufadhili maandamano ya kupinga Serikali yake,' sasa Serikali kupitia Wizara ya masuala ya kigeni imemtaka Rais wa Ford Foundation Darren Walker, kuwajibika na kutoa maelezo kuhusu fedha walizotuma kwa akaunti za mashirika na makampuni za Kenya kati ya Aprili 2023 na Mei 2024.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Serikali imedai kuwa Ford Foundation ilituma jumla ya Dola za kimarekani milioni 5.7, sawa na shilingi za Kenya milioni 752, kwa mashirika kadhaa yakiwemo:
Ikumbukwe Ford Foundation, iliyoanzishwa mwaka 1936 na Edsel Ford ambaye ni mwana wa Mwanzilishi wa kampuni ya Ford Motor Henry Ford, ilikanusha madai ya Rais William Ruto kuwa inafadhili maandamano ya kupinga serikali yake.

- Africa Uncensored Limited iliyopokea Dola 250,000.
- Women's Link Worldwide iliyopokea Dola 750,000.
- Kenya Human Rights Commission iliyopokea Dola 600,000.