Serikali ya Kenya yaipiga kufuli video ya Sauti Sol 'Melanin'

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598

Video mpya ya kundi la muziki kutoka Kenya Sauti Sol ft Patoranking 'Melanin', imefungiwa na serikali ya nchi hiyo chini ya bodi ya filamu Kenya (Kenya Film Classification Board KFCB)

Mkurugenzi wa bodi ya filamu Kenya Dr. Ezekiel Mutua, ametoa taarifa rasmi ikieleza kuwa imepokea malalamiko kutoka kwa watu kuwa haina maadili, na imetolewa bila kupitishwa kwenye bodi hiyo kuipa grade.

Pamoja na hayo bodi hiyo ambayo inasimamia ubora wa kazi za filamu nchini Kenya imevitaka vyombo vya habari kutocheza video hiyo, hsusan muda ambao watoto wanaangalia television.

Video mpya ya Sauti Sol wakimshirikisha Patoranking imeachiwa rasmi Novemba 20 mwaka huu, na mpaka sasa hivi tayari ina zaidi ya viewers laki 3 kwenye YouTube.


Muungwana
 
Nashukuru kuwahi siti pia ngoja niitazame
 
Hii video nimeiona ni
Moja kati ya nyimbo nzuri kutoka kwa saut soul, ila video yao hata mimi nilitilia shaka hiki kinachotokea, afadhari kule nyimbo zinafungiwa kwa kosa ka maadili huku kwetu zimbabwe ukitaka baraza la sanaa zimbabwe (BASAZI) lifungie nyimbo yako basi mponde mugabe uone utakavyo banwa map**bu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…