Serikali ya Kenya yatishia kuwafuta kazi madaktari na wahudumu wanaofanya mgomo

Serikali ya Kenya yatishia kuwafuta kazi madaktari na wahudumu wanaofanya mgomo

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Madaktari nchini Kenya wanaofanya kazi kwenye hospitali za umma wameungana na wahudumu wengine kwenye mgomo kulamamikia kutopewa bima ya afya na kufanya kazi kwenye mazingira magumu hasa katika kipindi hiki ambacho taifa hilo linapitia changamoto ya janga la virusi vya Covid-19.

Mgomo huu unakuja baada ya mazungumzo kati ya wawakilishi wa Madaktari na serikali nchini humo kugonga mwamba.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametishia kuwafuta kazi wahudumu walioamua kugoma.

Mgomo huu unakuja wakati huu nchi nchi hiyo inapoendelea kukabiliana na janga la Corona.

Kufikia sasa Kenya imerekodi visa 94,500 vya maambukizi ya virusi vya Corona baada ya visa vipya 349 kuthibitishwa na vifo 94,500 baada ya ya watu wengine 6 kuthibitishwa kufariki dunia kutoka na janga hilo hatari la COVID-19.

Watu 176 wameripotiwa kupona virusi hivyo na kufanya idadi ya jumla ya watu waliopona kufikia 75,735.
 
Kwani katiba malidhawa inasemaje watu wakitaka kugoma kidemokrasia kabisa?
Katiba yetu inaruhusu migomo. Serikali yetu pia inaruhusu migomo maana sisi ni demokrasia ya kweli. Lakini nyinyi migomo hairuhusiwi maana nchi yenu ni dictatorship.
 
Katiba yetu inaruhusu migomo. Serikali yetu pia inaruhusu migomo maana sisi ni demokrasia ya kweli. Lakini nyinyi migomo hairuhusiwi maana nchi yenu ni dictatorship.
Kama inaruhusu kwa nini wanatishiwa kufutwa kazi, au hujaelewa kilichoandikwa hapo?
 
Leo ni siku 16 ya mgomo wa wahudumu wa afya Kenya.
 
Kenya kuna shortage ya wasomi kada ya afya ndio maana hao wachache waliopo wanaindesha serikali wapendavyo.
 
Back
Top Bottom