Ubavu huo hauna, hapo Msumbiji Watanzania wamechinjwa juzi na kufurushwa na kunyang'anywa mali zao na hakuna chochote mlichokifanya, hata rais wenu nakumbuka akitoa kauli za kuunga mkono huo ufurushwaji, alishangaa nini mnafuata huko.
Binafsi nachukia sana kauli za Jaguar, ukizingatia ni msanii pia na nyimbo zake hupendwa Tanzania, sijui alikua amelewa kitu gani, hizi kauli za kubaguana sio nzuri.
-------------------------
Takriban raia 132 wa Tanzania wanaoishi nchini Msumbiji wamefurushwa nchini humo huku wengine wasiojulikana wakidaiwa kukamatwa kufuatia operesheni ilioanzishwa na serikali ya taifa hilo.
Kulingana na serikali ya Msumbiji operesheni hiyo inalenga kuwatimua raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.
Taarifa ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki nchini Tanzania imesema kuwa raia waliofukuzwa ama hata kukamatwa ni wale wanaoishi mji wa Monte Puez kwa kuwa una raia wengi wa kigeni ikilinganishwa na miji mingine.
Kulingana na taarifa hiyo tayari ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji unaendelea kufanya mawasiliano ya kidiplomasia na serikali ya Msumbiji ili kuwahakikishia usalama raia wa Tanzania na mali yao nchini humo.
Inakadiriwa kuwa, Watanzania wapatao elfu tatu (3,000) wanaishi na kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii katika mji huo wa Monte Puez.
Hatua hiyo inajiri licha ya mataifa ya Msumbiji na Tanzania kufanya mkutano wa kuainisha maeneo ya ushirikiano yakiwemo maswala ya kibiashara na uhamiaji.
Na huku operesheni hiyo ikiendelea serikali ya Tanzania imekuwakumbusha Watanzania wote waishio ughaibuni, kufuata Sheria na taratibu za nchi hizo wanazoishi.
Kulingana na serikali ya Msumbiji operesheni hiyo inalenga kuwatimua raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume na sheria.