Serikali ya kijeshi ya Chad imetoa msamaha kwa karibu waasi 300 pamoja na wapinzani

Serikali ya kijeshi ya Chad imetoa msamaha kwa karibu waasi 300 pamoja na wapinzani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Serikali ya kijeshi ya Chad imetoa msamaha kwa karibu waasi 300 pamoja na wapinzani, ikiwa hatua kubwa kuelekea shinikizo kutoka kwa makundi ya upinzani yaliyoalikwa kuhudhuria kikao cha pamoja cha kujadili hatima ya kisiasa ya taifa hilo lenye matatizo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, msamaha huo ni kwa watu 296 waliokuwa wamezuiliwa kutokana tuhuma mbali mbali zikiweno za kutoa maoni, ugaidi pamoja na kuhujumu serikali .

Makundi ya upinzani yamesema kwamba msamaha huo ulikuwa moja wapo ya masharti kabla ya kuhudhuria kikao cha pamoja kilichopendekezwa na rais Mahamat Idriss Deby Itno mwenye umri wa miaka 37 aliyechukua madaraka baada ya baba yake Idriss Deby Itno kuuwawa wakati wa mapambano na wanamgambo mwezi Aprili.

Wakazi wengi wa mji mkuu wa N'Djamena wanasemekana kufurahishwa na msamaha huo wakiuelezea kama hatua ya kwanza kuelekea kuliunganisha taifa.

Kelma Manatouma ambaye ni mtafiti wa masuala ya siasa kutoka chuo kikuu cha Nanterre karibu na Paris, ameiambia AFP kwamba hiyo ni hatua muhimu kuelekea maridhiano pamoja na kukubalika kwa uhalali wa utawala wa Deby.

VOA Swahili
 
Back
Top Bottom