Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Ni jambo lisilo la kawaida kutokea katika zama hizi, ambapo huko Mbeya Vijijini, Serikali ya kijiji cha Mashese kata ya Ilungu imegharamia bima za afya kwa zaidi ya wananchi 1,500 kwa shilingi milioni 10 ili kuhakikisha huduma za afya kwa jamii.
Mwenyekiti wa kijiji, Osia Lazaro Mwakalila, amesema lengo ni kuwafikia watu 2,000, wakiwemo wanafunzi na wakazi walioko nje ya kijiji.
"Serikali ya kijiji (Mashese) tulipokaa tukaangalia kutokana na vyanzo vyetu vya mapato ya kijiji tukaamua kuwakatia bima za afya wananchi na lengo letu ni wananchi wote wapate bima kwasababu wengi hawana kipato tukitembelea wananchi huko tukaona wanaumwa halafu hawana hela. Tunachoomba Serikali na wadau watusaidie vifaa vya maabara kuja hapa Zahanati ya Ilungu na pia wadau wakiwemo waliotoka hapa Mashese tunatamani hili liwe endelevu", amesema Osia Mwakalila, mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Mashese kata ya Ilungu Mbeya vijijini.