Haujawahi kusikia watu wanamlaumu Nyerere hadi leo kwa mambo ambayo wamekua na nafasi ya kuyarekebisha?
Hii naona ni kisingizio tu, mbaya zaidi hata yeye mwenyewe Mama alikiri hadharani kwamba yeye na JPM ni kitu kile kile, hapo alieleweka japo baadhi ya mambo aliyoyafanya yalipingana na kauli yake.
Kwenye hiyo inayoitwa serikali ya JPM wote walikuwepo na walishika nafasi za juu ikapelekea wakamate uskani wa nchi. Unaposema kuondoa uongozi wa JPM sijajua unataka usimike upinzani na ufumue kuanzia chama tawala au ni kubadili watu wote waliopo madarakani?
Nimeona hata TL amesema kweli jemedari na ukatili wake lakini hakuwahi kuwabambikia watu kesi za ugaidi. Nikasema kweli siasa na ukahaba tofauti ni bidhaa tu, lakini siasa ni zaidi ya ukahaba. Usimwamini mwanasiasa yeyote.
Acha tusubirie wajuvi waje kutupa darasa mkuu.