Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Katiba Inayopendekezwa!!

Mwakaboko King

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2015
Posts
1,099
Reaction score
207
Ndugu wana jamvi naomba nilete hoja hii inayoizungumzia SMZ na Mamlaka yeke kwa uzuri kabisa kwenye Katiba Inayopendekezwa!

Ibara ya 163-(1) Inatamka wazi kuwa na Serikali ya Zanzibar itakayojulikana kama SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ambayo itakua na mamlaka katika Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano kwa mujibu wa mashati ya katiba hii.
(2)Bila kuathiri masharti ya yaliyomo katika Ibara hii na katika Ibara zifuatazo katika sura hii,Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaundwa na kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

IBARA YA 164 (1) Inaeleza kuwa kutakuwa na Rais wa Zanzibar ambaye atakuwa Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar atakayechaguliwa kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya 1984.

kifungu cha 2 kinaeleza kuwa Raisnwa Zanzibar kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa Zanzibar kiapo cha kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano, na kiapo kingine chochote kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar kinachohusika na utendaji wa kazi yake , kisha atashika na kutekeleza madaraka hayo kwa mujibu wa Katiba hii na Katiba ya Zanzibar.

Naomba kuwasilisha!!!!
 
Kwa hili hakika kura ya Ndiyo haiepukiki hata kidogo, naamini baadhi ya watu mambo haya hawayajui na wanabaki kuipinga tu pasipo kujua.
 
Back
Top Bottom