Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar yazindua meli Mpya ya mafuta

cblhbn

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2015
Posts
394
Reaction score
494
Raisi wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dr Mohamed shein, amezindua meli mpya kwa ajili ya usafirishaji wa mafuta, kufwatia ahadi iliyotolewa kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Ilani ya chama cha mapinduzi (2015 -2020), ilitanabahisha serikali itanunua meli zipatazo 4 ili kuweza kurahisisha uchakataji na usafirishaji wa mafuta, meli mpya ya mv ukombozi II, imekua meli ya sita kuagizwa na serikali ya Zanzibar, kupitia fedha za ndani, ambapo ahadi na uhitaji halisi ulikua ni meli nne Kama ilani inavyosema.
Meli hizi zitachochea uchumi wa Zanzibar na jamhuri ya Tanzania kupitia biashara ya mafuta na gesi. Raisi Shein amesema swala la uchakataji wa mafuta ni biashara kubwa sana duniani na yenye tija kiuchumi na sio la kukurupuka
#hapanikazituu
#Tanzanianikazituu
#sijuiwenginenikazinini
 
Itawasaidia kupunguza uhaba wa mafuta Zanzibar na safari za mara kwa mara kuja kufata mafuta Dar.
 
Itawasaidia kupunguza uhaba wa mafuta Zanzibar na safari za mara kwa mara kuja kufata mafuta Dar.
Kweli brother, Na Kwa ukanda huu wa Africa mashariki, Zanzibar ndio inaongoza kwa usajili wa meli nyingi, na siku Zanzibar ikianza kuuza na kusafirisha itakua ni non-stop
 
Kweli brother, Na Kwa ukanda huu wa Africa mashariki, Zanzibar ndio inaongoza kwa usajili wa meli nyingi, na siku Zanzibar ikianza kuuza na kusafirisha itakua ni non-stop
Zanzibar wanaongoza kwa usajili wa meli. Na serikali yao inamiliki meli kama hii iliyokuja sasa.
 
Hii ina uwezo wa kubeba tani 3000 itakuwa inachukua mzigo kutoka kwenye meli kubwa zinazo leta mafuta huku kwetu.
 
Wengine walinunua kiwanda cha samaki wakapea Navy.
 
Zenji napakumbuka sana, uzuri wenu hamnanga chuki, mnajua kuishi na Wakenya vizuri, Wakenya wanaochapa kazi na biashara Pemba na Unguja husifu sana hicho kisiwa, nawatakia kila la kheri kwenye jitihada zenu. Tatizo huko kwenu dah raha yaani kazi huwa ngumu sana kufanyika, nilikua nashindwa kuvumilia, kila jioni lazima tutoke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…