benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Rais wa Marekani, Joe Biden amejaribu kuwahakikishia Viongozi wa Ulimwengu kuwa Marekani haitoshindwa kulipa deni lake licha ya kiwingu kinachogubika mazungumzo ya kuongeza ukomo wa Serikali yake kukopa.
Akiongea kabla ya kukutana na Viongozi wa kundi la Mataifa manne linalofahamika kama QUAD pembezoni mwa mkutano wa G7 huko Hiroshima nchini Japan, Biden amesema hakuna sababu ya ulimwengu kuwa na wasiwasi juu ya deni la Marekani.
Amesema anaamini mazungumzo yanayoendelea kati yake na Wabunge wa Republican yatazaa matunda huku akitolea mfano kuwa duru ya pili na ya tatu ya mazungumzo hayo yamepata mafanikio fulani ya kutia moyo.
Serikali ya Biden inatanga kuongeza uwezo wake wa kukopa kufikia dola Trilioni 31.4 lakini Wabunge kutoka Chama cha Republican wanapinga mapendekezo hayo kwa hoja kwamba deni la Nchi hiyo tayari limefikia kiwango cha kutia wasiwasi.