Serikali ya Mpito, ipo au haipo

Serikali ya Mpito, ipo au haipo

Singo

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Posts
1,204
Reaction score
1,143
Wasalaam,

Nimehamasika kuja na uzi tajwa baada ya kumsikia mama rais Samia akionesha kushangazwa na kusikitishwa na minong'ono iliyokuwepo bungeni kipindi kile baada ya aliyekuwa rais wa Tanzania JPM kufariki dunia

Kwa mujibu wa mama,ilimbidi kusoma katiba na hakaona kitu kinachoitwa serikali ya mpito ktk katiba ya nchi ,hivyo anaamini walioanzisha minong'ono hiyo walikuwa na ajenda ya kujipanga kuchukua nafasi yake aliyoipata kikatiba baada ya rais kufariki hapo 2025, na yeye binafsi haafikiani na walionzisha minong'ono hiyo.

Swali ninalojiuliza ,ikiwa rais aliyepo madarakani akafariki na katiba ikasema, Makamu wa rais anachukua nafasi hiyo mpaka muda wa awamu yule aliyefariki utapotimia ,je hii haiwezi tafsiriwa kama ni serikali ya mpito(kwamba makamu amekuwa rais kikatiba kumalizia muda wa yule aliyefariki)

Tuchukulie mfano hayati rais Magufuli angefariki mfano 2025 mwezi wa May maana yake angekuwa amefariki kabla ya muda wake kuisha na makamu wake wa urais angekuja chukua nafasi ya urais kwa miezi iliyobaki , je huo muda ambao angedumu huyu rais mpya ni kosa kuita muda wa mpito yaani kumalizia muda wa rais aliyefariki.

Sasa ikiwa muda wa makamu aliyeingia kushika nafasi ya urais baada ya rais kufariki ukafika mwisho, katiba inasemaje kuhusu , yeye kugombea nafasi ya urais tena na awamu yake itambulikaje.je mfano akaita ni awamu ya sita,yaani inaendeleza hii awamu aliyoanza kuwa rais kikatiba 2021, vipi ikatokea wakashinda upinzani awamu yao itaitwaje

Kama katiba haijaweka mambo kwa uwazi huhusu serikali ya mpito nk ,kipi kinatakiwa kifanyike ili kuondoa hali ya sintofahamu.
 
Ni serikali ya mpito iliyopatikana kidemokrasia. Ni uelewa na panic tu.
 
Back
Top Bottom