Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Serikali mkoani Singida, imeonya wafanyabiashara watakaopandisha bei za vyakula kuelekea mfungo wa Ramadhani, kwa Waislamu na Kwaresma kwa Wakristo, huku ikisema haitavumilia hatua yoyote ya kujinufaisha kipindi hicho, kwa gharama kubwa ya wananchi.
Soma Pia: Mufti na Sheikh Mkuu Abubakar Zubeir: Mwezi haujaonekana, mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan utaanza Jumapili March 02,2025
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 1, 2025, ofisini kwake, amesema Serikali inataka kuona bei za bidhaa za chakula zinaendelea kubaki katika viwango vya kawaida, na kuonya kwamba, yeyote atakayekaidi, atakabiliwa na mkono wa sheria.