Serikali ya Tanzania kuweka vituo vya kufundisha Kiswahili kwenye Balozi zake

Serikali ya Tanzania kuweka vituo vya kufundisha Kiswahili kwenye Balozi zake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Serikali nchini imeagiza uwepo wa vituo rasmi ya kujifunzia lugha ya Kiswahili katika nchi zenye balozi lengo likiwa ni kupanua matumizi ya lugha hiyo kimataifa.

Akizungumza leo bungeni jijini Dodoma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hatua hiyo itasaidia kufungua fursa za kiuchumi ikiwemo kuwaajiri watanzania ambao watakuwa walimu wazuri kwenye ufundishaji wa lugha hiyo.

“Tunapokwenda kuwa waalimu tayari tunafungua fursa kiuchumi kuwaajiri watu, watanzani kwenda kufanya kazi na kodi itaongezeka.”amesema Majaliwa
 
Nchi ya maajabu, mmeshindwa kujenga viwanda mlivyoshadadia kama watoto wa chekechea, leo maona mtawateka "wajnga" kwa ngonjela za Kiswahili as if sheria zikiandikwa kwa Kiswahili uchumi wa nchi utachupa.

Sasa nguvu yote ni Kiswahili, kiswahili Kiswahili! Mwijage akaja na "ujinga" eti cherahani ni Kiwanda, na "wajinga wakashangilia.

Kiswahili kipo, kitaendelea kukua na si cha kushadadia kama vile ndio nguzo ya uchumi wetu.
 
Leo hapo Morogoro
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Anazindua Kiwanda Cha Ngozi
 
Ukiwa hauna uchumi mkubwa then hakuna mtu atakua na shobo ya kujifunza lugha yako.

Wachina utajifunza lugha yao utake usitake maana unaenda kuchukua mzigo wa dukani kwako huko China, je wageni watajifunza Kiswahili kwa wingi ili wapate nini?
 
Back
Top Bottom