Serikali ya Tanzania yasema kuna visa 519 vya kipindupindu, kati yao wagonjwa 11 wamefariki mwaka 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Takwimu za Wagonjwa wa Kipindupindu Nchini Tanzania kuanzia Januari 2022 hadi Agosti 2022 ni visa 519 ambapo kati yao 11 wamefariki Dunia, Mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma ikitajwa kutoa wagonjwa wengi.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri kusimamia sheria za usafi wa mazingira ili kudhibiti na kuzuia mlipuko wa ugonjwa huo.

“#Kipindupindu ni Ugonjwa wa masikini, na unaendezwa kwa njia kubwa mbili ambazo ni maji au chakula kisicho salama.

“Aidha, takwimu zinaonesha Afrika inachangia 20% ya maambukizi ya ugonjwa huo Duniani, pia inachangia 80% ya vifo vya Kipindupindu,” – Ummy Mwalimu.
 
Hizi habari ziliishaga kipindi cha JK, zinarudi tena, duuuh!
 
Kipindupindu ni miongoni mwa magonjwa ambayo husababishwa na aina ya bakteria aitwaye Vibrio cholerae, Ugonjwa huu ni wa kuambukizwa kwa njia ya viini vinavyoenezwa kupitia kwa kinyesi kutoka kwa wagonjwa wenye Kipindupindu.

Kipindupindu (cholera) kimerudije Tanzania wakati tulikisahau?

Hakuna usimamizi wa usafi, mazingira na afya wenye nidhamu ndio maana haya yote yatatokea mpaka tauni itarudi kwa uzembe wa kila mmoja

http://whqlibdoc.who.int/hq/2004/WHO_CDS_CPE_ZFk_2004.4_swa.pdf
 
Takwimu za Wagonjwa wa Kipindupindu Nchini Tanzania kuanzia Januari 2022 hadi Agosti 2022 ni visa 519 ambapo kati yao 11 wamefariki Dunia, Mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma ikitajwa kutoa wagonjwa wengi.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri kusimamia sheria za usafi wa mazingira ili kudhibiti na kuzuia mlipuko wa ugonjwa huo.

“#Kipindupindu ni Ugonjwa wa masikini, na unaendezwa kwa njia kubwa mbili ambazo ni maji au chakula kisicho salama.

“Aidha, takwimu zinaonesha Afrika inachangia 20% ya maambukizi ya ugonjwa huo Duniani, pia inachangia 80% ya vifo vya Kipindupindu,” – Ummy Mwalimu.
Mwaka wa Tabu ni shida
 
Back
Top Bottom