JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
NAIBU WAZIRI WA AFYA, Dkt. Godwin Mollel (Mb) amesema, mnamo tarehe 20 mwezi Septemba, 2022 Wizara ilipata taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda. Taarifa ilieleza mgonjwa aliyethibitika kuwa na ugonjwa wa Ebola amefariki wilayani Mubende nchini Uganda.
Taarifa hizo zilionesha kuwa na dalili za homa kali, degedege, kutapika matapishi yenye damu, kuharisha na kutokwa damu machoni.
Taarifa za uchunguzi zinaonesha ugonjwa huu umesababishwa na kirusi cha Ebola aina ya Sudan (Ebola-Sudan strain). Uwepo wa ugonjwa huu katika nchi jirani unaiweka nchi yetu katika hatari kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu kupitia mipaka ya nchi kavu, viwanja vya ndege na bandari.
Dalili kuu za ugonjwa huu ni pamoja na homa kali, inayoambatana na kutokwa damu katika matundu ya mwili yaani pua, njia ya haja kubwa na ndogo, mdomoni, masikioni na machoni, hali inayopelekea kifo kwa muda mfupi. Ugonjwa huu unaenea kwa kugusa majimaji ya mwili wa mgonjwa mfano mate, damu, mkojo na machozi.
Endapo utapata au kuona mtu mwenye dalili hizi, unashauriwa kuwahi kituo cha kutolea huduma za afya mapema.