SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO CHA MIPANGO. hivi karibuni tumefanya uchaguzi wa serikali ya wanafunzi Mi

SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO CHA MIPANGO. hivi karibuni tumefanya uchaguzi wa serikali ya wanafunzi Mi

Twevel

New Member
Joined
Jul 8, 2013
Posts
1
Reaction score
0
Hivi karibuni tumefanya uchaguzi wa serikali ya wanafunzi Mipango. Watu walijawa na furaha kubwa kama vile wamepata kiongozi makini na shupavu. kwa upande wangu ni kama kukomboa kuku kwa ngombe. Dalili za ufisadi zimeonekana mwanzoni kabisa kwa raisi huyo mpya.
Amechagua baraza karibu asilimia 90 nje ya wabunge wa kuchaguliwa. hii inamaanisha kuwa alisha panga baraza lake hta kabla ya kuchaguliwa madamu tu wamsaidie kampeni.
Pili spika wa bunge ametokana na mbunge wa kuteuliwa, je alijuaje kwamba atateuliwa? na kuchukua hatua ya kuandika barua ya kuomba Uspika, hii ni michezo michafu iliyoonekana katika uongozi wa kinda huyo.
wabunge walibaki kushangaa tu, hakuna aliyehoji hilo.
yote haya ni matokeo ya katiba isiyokuwa ya wanafunzi bali ilipitishwa na nguli mmoja tu. ndio maana uchaguzi mwaka huu ulipita kwa matatitzo makubwa sana.
katiba imempa rais nafasi kubwa mno ya kupendekeza idadi apendayo yeye wabunge wa kuteuliwa. katika hao mawaziri, wapo waliopewa wizara nyeti ambazo ama hakika kwa jinsi tuwajuavyo ni mzigo kwao.
wizara kama za elimu, mikopo, tunataka kukipeleka wapi chuo chetu? FIKIRIENI HILO. KWAKUWA AMEJAZA MARAFIKI ZAKE KWENYE BARAZA HILO, HATAKUWEPO WA KUMPINGA KATIKA LOLOTE WAKATI WOWOTE. tutajikomboa lini na uovu wa viongozi chuon petu, naomben wanajamii forum tujadili hilo.:kev::kev:
 
Back
Top Bottom