Serikali ya wanyonge inapanga bei elekezi kwa ajili ya bidhaa za viwandani, lakini kwa makusudi imeamua kuwapuuza na kutowajali kabisa wakulima

Serikali ya wanyonge inapanga bei elekezi kwa ajili ya bidhaa za viwandani, lakini kwa makusudi imeamua kuwapuuza na kutowajali kabisa wakulima

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Japo kwa miaka mingi Tanzania tunajisema kilimo ni uti wa mgongo, ukweli ni kwamba wakulima katika nchi hii ndio kundi la mwisho kukumbukwa na serikali. Tunafanya maendeleo ya mijini, kununua ndege, kujenga flyover nk, vitu ambavyo havimgusi sana mkulima wa kule kijijini.

Wakulima wanaishi vijijini. Bado barabara za kwenda vijijini waliko wakulima hazipitiki wakati wa mvua, bado wakulima wanatembea mwendo mrefu kufuata huduma za afya, bado wakulima wanatapeliwa na na wachuuzi katika kuuza mazao yao, bado wanawake na watoto wanakufa kwa idadi kubwa kwa kukosa huduma za afya bora huko vijijini, bado vijijini kwa wakulima kuna michango na kodi za ajabu ajabu, bado wakulima wa vijijini wanaonewa sana na watendaji, lakini serikali haina hata mkakati wa kuwasaidia.

Sasa Magufuli anaposema serikali yake ni ya wanyonge, wanyonge wepi, hawa wahuni wanaoishi mijini?

Mara ngapi tunaposafiri vijijini tunanunua bidhaa za wakulima, mara nyingine wanawake wazee wanaotoa jasho kupata hela ya ada za shule na chakula za wajukuu wao, kwa bei ambazo tunajua kabisa tunawaonea? Unapita maeneo yenye ndizi, unaambiwa mkungu wa ndizi kwa Shs 1500, na bado unalalamika upunguziwe bila kujiuliza huyo bibi mzee anahitaji hela kwa ajili ya kitu gani, hela abayo kwako wewe ni ya kununua soda tu ukiwa Dar, ambayo yeye hakumbuki mara ya mwisho alikunywa lini kwa kuwa soda kwake ni luxury item!

Serikali inakuwa makini sana kupanga bei elekezi, za mafuta, sukari, simenti nk. Je, serikali imewahi kujiuliza kama wakulima wanauza mazao yao kwa bei ambayo angalau itarudisha gharama zao za kuyalima? Ni wazi hakuna anaejali, si Magufuli, si Wizara ya Kilimo, si wabunge. Unajua kwa nini? Kwa sababu hawa watu ndio wanaofaidika na bei za barabarani za mkungu wa ndizi kwa shs 1000, hivyo hawataki kuingilia.

Ni lini basi serikali itakuwa na utaratibu Halmashauri kuwa na bei elekezi za ununuzi wa mazao ili angalau wakulima warudishe mitaji wanayotumia katika kulima hayo mazao? Hili ni jambo la kufanywa katika ngazi ya Halmashauri, sio taifa. Ikibidi serikali ichukue jukumu la kuanzishwa kwa Sacco za wakulima katika kila Halmashauri.

Tunajua serikali ilifanya makosa makubwa kwenye kutaka kusimamia ununuzi wa korosho miaka miwili iliyopita. Lakini makosa yaliyosababishwa na Magufuli kutotaka kusikiliza ushauri na maoni ya watu wengine yasifanye asitake tena kuwasaidia wakulima katika suala la bei ya mazao yako. Kwa kosa lililofanywa na Magufuli, wakulima hawapaswi kuadhibiwa.
 
Unapita Kiwira Tukuyu, unaambiwa na huyu mama kachoka kuwa bei ya huu mkungu wa ndizi ni Shs 2000, unalalamika uuziwe kwa shs 1500! Serikali haijali.

1607417516659.png
 
Unaambiwa bei ya ungo wote wa ndizi ni 1500 ili angalau hawa wanawake wapate hela ya ada za shule na kuwanunulia watoto waliowaacha nyumbani chakula cha jioni. Unataka uuziwe ungo wote kwa shs 1000 ambayo hata bia yako moja hiyo hela hainunui! Kuna haja serikali kuanza kungilia haya mambo.

1607417755405.png
 
Je, unafikiri hawa kina mamam wanabahatika kupata mteja kila siku ili angalau wapate hela ya kula? Inapotokea bahati ya wewe kuwa mteja, unataka uwape bei ya kuwanyonya na kuwanyayasa. Je, ndio hawa wanyonge wanaofaidika na ndege zetu dreamliners na flyovers?

1607417979246.png
 
Hawajatilia mkazo nyanja hizo... mkazo wao upo kwenye kukuanya kodi...




Cc: mahondaw
 
Tufyatuwe watoto wengi vita panda bei tu!
Wakifungua mipaka viuzwe nje bei itakuwa nzuri kwa wakulima
 
Tufyatuwe watoto wengi vita panda bei tu!
Wakifungua mipaka viuzwe nje bei itakuwa nzuri kwa wakulima
Hakuna biashara ngumu Tanzania kama kuuza mazao nje ya nchi. Ukiambiwa mlolongo wa vibali utazimia. Halafu huwa ni vibali vya muda mfupi.
 
Hakuna biashara ngumu Tanzania kama kuuza mazao nje ya nchi. Ukiambiwa mlolongo wa vibali utazimia. Halafu huwa ni vibali vya muda mfupi.
Hapo ndipo wanapo waumiza wakulima tuna safari ndefu sana chini ya CCM hawataki wakulima wapate pesa wata peleka watoto shule nzuri watakuja kuwa challenge!!
 
Hapo ndipo wanapo waumiza wakulima tuna safari ndefu sana chini ya CCM hawataki wakulima wapate pesa wata peleka watoto shule nzuri watakuja kuwa challenge!!
I say, sikuwahi kufikiria hilo! Mwanadamu ni mnyama kwa kweli!
 
Back
Top Bottom