Jaya_lchemist
Senior Member
- Oct 12, 2022
- 123
- 207
Serikali ya Wezi, Taifa la Waliodanganywa S01 Episodi 01
*********Ni Alfajiri hapa Mwiki,Kasarani jijini Nairobi. Alfajiri hii ni kama zile alfajiri nyingine nyingi za mwaka. Alfajiri hii haifanani na zile alfajiri za mwezi Julai. Julai, mwezi ule kila mtu analalamika kuwa baridi kawa baridi. Eti baridi sasa maana yake kamili inajulikana mwezi huu. Sasa maana ya alfajiri kujiri inaonekana na kushuhudiwa na kila mwenyeji hapa. Nimetumia neno mwenyeji kwa sababu mimi mgeni hapa. Ninashuhudia wenyeji wafanyabiashara wakianza kuzifungua biashara zao, huyu anatoa karai kutoka ndani ya duka anaiweka nje juu ya display yake, huyu anawasha jiko la makaa hapa ile ayaweke mafuta ya mandazi yaanze kuyeyuka ile ayachome maandazi. Yule naye kachukua mkokoteni anaanza kuuvuta kana kwamba ataishi kuuvuta milele daima- la wacha niseme hata wakati ule Mwokozi Yesu atarudi kuchukua Wacha Mwana na Mungu Mkuu.
Uchangamfu ndio unaotawala eneo hili. Kisa? Siku ikianza ni dalili ya jambo jema kutendeka. Wateja kuja, wateja kuleta wateja wengine, labda ule kiongozi wetu Mtukufu Rais Ruto atasusha gharama ya maisha. Lakini kwangu mimi naona hii ni ndoto. Naam zile ndoto tunajilazimisha kuamini zitatendeka ilhali dalili zote zinapinga ndoto kuwa kweli. Kwa nini niseme ni ndoto? Kwa nini nisiamini katika ndoto za wafanyabiashara kuwa Rais atabadilika? Abadilike vipi na tabia ni ngozi. Ameishi kuwa hivi toka enzi za Rais Moi. Wao walikuwa ndugu wa toka nitoke. Mwalimu na mwanafunzi wake, mwizi mahiri akimfunza mwanafunzi wake kanuni na taratibu za wizi. Naona ukijiuliza kwani wizi una kanuni na taratibu kama zile za nchi, zile za katiba ile ya 2010? Naam wizi una kanuni zake na taratibu. Ungekuwa wizi vipi bila kanuni. Tungemtambua vipi mwizi hodari na yule ambaye wizi aliuanza juzi. Huyu hodari anamwiba mama aliye na mtoto hadharani bila aibu. Anamtazama mtoto mdogo aliye mgongoni mwa mamaye anavyolia. Anageuza macho yake kwa mamaye na kuongeza uzito wa sauti yake,” Mama mtoto leta simu na cash uliyo nayo.” Mama anadondokwa na machozi, kitoto kama kinachojua mamaye ananyanyaswa kinaongeza nguvu na sauti ya kilio. Hili litamfanya pwagu au tumwite pwaguzi apate hata tone la hurume? Kama anayetupa jibu la swali letu, anatumbukiza mkono mfukoni wa jeans yake iliyochapa. Mkono unatoka ukiwa umenasa jisu lililojaa kutu. Mama anapiga nduru kali, kitoto hakilii sasa kinaomboleza kwa sauti inayoweza kumwamsha Mtukufu Rais wa kwanza wa Taifa kuu la Kenya.” Leta ganji na tenje haraka ama nimchinje mwanao!” Mama anatoa keshi na Smartphone na kumpa mnyama huyu asiye huruma.
Kwa hivyo, wizi ni kama mchezo. Kila mchezo una kanuni zake, kadanda ina kanuni moja kuu- piga pasi ukitumia miguu peke yake, usiutumie mkono au mikono kamwe, voliboli pia, chess vilevile imejaa kanuni. Kwa hivyo mchezaji mahiri wa kadanda ni ule anayezifuata kanuni za kadanda na ameziandika kanuni hizo moyoni. Kuna wale hata baada ya kuzijua kanuni wanazifuata kisha wanaona hawapati matokeo wanayoyapenda. Hili linazaa juhudi za wizi na kusoma mchezo huu kwa undani zaidi. Wanakosa kula, kunywa, kwenda haja ili wajue kuuiba mchezo huu. Mazao ya juhudi zao yataonekana Jumamosi katika mashindano baina ya Timu yao na Timu pinzani. Yetu macho tu,kimya.
Lakini mbona tuishi kimya? Pwagu na pwaguzi, mwizi mahiri na mwanafunzi wake wanaendelea kuishughulikia njaa yao ya utajiri. Baada ya kushiba na kutajwa kwenye orodha ya matajiri nchini na Afrika, hawatosheki. Kama vile mwandishi wangu kipenzi, Ben Ramadhan Mtobwa, anavyosema kuwa hawa baada ya kuikata kiu ya utajiri wanaendelea kuilinda shibe hiyo. Mungu ailaze roho yake pema peponi!
Ama tukae kimya tungoje wakati wa Yesu Kristo, wakati wa Jehova Mungu Mkuu? Huku mimi na wewe tukiomba na kuamini kuwa Shibe Itawamaliza. Lakini mbona tuwaombee mabaya wakati Messia alituasa tuwaombee mema maadui zetu? Hawa ni maadui wetu. Maadui wa Taifa la Kenya. Toka zile enzi za Shujaa Dedan Kimathi alipoikomboa nchi. Toka zile enzi tulimvika urais msaliti aliyeisaliti Maumau. Aliyelisaliti Taifa lake akavikwa Shujaa namba wani. Tukampa zawadi ya kutuongoza aliyewapa wazungu wazungukaji Dedan Kimathi kama kafara. Kwa nini tulifanya hivi? Kwa nini wakenya hawakuelewa kilichoendelea? Wakati wakimkebehi na kumtukana Ndirangu Mau aliyempiga Dedan Kimathi risasi tarehe Octoba 21, 1956, tunampigia makofi yule aliyemsaliti. Hatubaki hapo, tunamvika mwanae msaliti huyu urais. Nielewe, sina ugomvi na mwana mimi. Mimi siamini kuwa mbegu mbaya ya mzazi ina asilimia mia moja ya uweza wa kumdhuru mwana. La! Nimewashuhudia mashetani ya wazazi yakiwazaa malaika wanaomwabudu Jehova na Roho Mtakatifu na Mungu Mwana kwa roho na kweli. Mwana hafai kuadhibiwa makosa ya mzazi. Mimi kamwe sina shida na uongozi wa mwana. Wale wezi mahiri ndio wanaoyoyakereketa maini yangu. Wale bweha waliovaa ngozi ya kondoo. Hata bweha wengine bila aibu, wanaenda kwenye taifa ya wanakondoo na kusimama kandamnasi.”I promise I will be a Vegetarian!” Vegetarian anavikwa uongozi na wanakondoo waliokosa kumcha Jehova na Mwanaye. Waliokosa kumsihi Mwenyezi Mungu awape kiongozi. Kama zile enzi za Daudi, Sauli na Wanaisraeli, Mungu anamchagua kiongozi. Wanaopiga magoti na kumsihi Jehova awape Rais watamwona akiwapa Daudi au Solomoni. Lakini wanataifa wakikosa kumsihi Mungu awape kiongozi, watamchagua Sauli. Wanamchagua vegetarian. Kisa? Alilia mbele yao na kuwapa matumaini na fake promises. Mimi ni rais wa wanyonge. Bottom up!!! Mazao ya maamuzi yao, anazitoa kucha zake akiupata urais. Anaanza kumla kondoo mmoja baada ya mwingine huku akiwa kwenye Telly akiwapa wanakondoo fake promises. Wale wenye hekima watanielewa kwa kina ninachomaanisha sio kondoo wanaomwamini bweha vegetarian mbele yao.
********
Sasa fikra zinarudi kwenye nganya hii ya Kanairo. Haya mawazo yote yaliibuka nilipowaona wafanyabiashara wa kiike kwa kiume wakichapa bizna vilivyo.
Sasa watu wameongezeka kwenye nganya hii. Bikizee sasa ameketi nami sako kwa bako. Viti vilivyo kando yetu vimewahifadhi mtu na mpenziwe. Hawa walianza kwa mzaha. Huyu wa kike akiutalii mwili wa boyfriend wake. Alianza kwa kuviteleza vidole toka kwenye shingo yake. Boyfriend naye kakaa kama ambaye hajaguswa kimahaba na beb wake. Ama hisia zake ziko mbali sana kutoka kwenye ulimwengu wa mahaba ama anaona aibu kujibu mguso wenyewe mbele ya ajuza aliye kando yangu. Binti wa watu hatulii. Anaupeleka mkono kifuani mwa babe. Hapa anakaa kwa sekundi asilimia kumi na tano. Beb naye katulia kama maji mtungini. Msichana hafi moyo aliutelezesha mkono wake hadi kwenye mapaja ya mpenziwe. Jitu sasa limeanza kujibu miguso. Linaanza kumshika msichana wa watu nywele. Knotless braids zinapelekwa mbele, sasa zinalalia kifua cha binti. Anapata nafasi kwenye shingo. Anaulaza mkono hivi kwamba vidole vyote vinne vimemnasa babygal shingoni kwa nyuma. Namtazama ajuza alivyozubaa. Sasa mdomo wa boyfriend unasafiri upatane na wa beb ama tumwite babygal. Binti Sasa ako kwenye dunia yake. Mtego alioutega sasa umefyatuka. Anaanza kuguna. Hapa wacha niseme kama alivyosema Lil Wayne kwenye ngoma itwaayo Corazon: “French kissing like they in Paris.” Ajuza sasa aliwacha kuzubaa. Sasa alianza kutukana:”Vijana wamekosa adabu!” Wapenzi hawasikii ama labda walimsikia lakini wakaamua kumpuuza. Aliona hilo halifanyi kazi sasa alianza kumwomba Mwene Nyaga. Hilo halikutosha, kamnyang’anya binti aliye mbele yetu Mango Delmonte aliyoishika kama washikavyo martini glass ya Cocktail pale kwenye klabu. Kafungua dirisha kaimwaga nje ya nganya. Kasonya alipoona imemwagika kwenye cabro blocks pale kwenye stop ya mat na hizi nganya. Kafyatuka nje kakimbia asilimia mita kumi na tano na kuimwaga Delmonte kwenye mchanga. Kaanza kumwomba Mwene Nyaga.
Binti aliyenyang’anywa Cocktail yake sasa siye binti mpole niliyemwona sasa namwona kageuka kawa kama yule Mitchelle Mjaka Mfine wa TikTok. Kawa kama yale majimama ya coast yanayoamka na kuifunga dera vizuri ili wavamiane kama majichui mawili ya vijike. Baluni ambazo ni kama hazijapulizwa ziliyo kifuani sasa zinaenda mbele nyuma kama ile pendulum ya Physics pale Highschool. Kasi kamwendea bikizee. Watu sasa wanashuka mmoja baada ya mwingine washuhudie. Jeshi ya Nduthi ama tuiite boda sasa wameziamkia nduthi zao waione sinema vizuri. Jimama kando yangu mlangoni mwa nganya linasema “Netflix ni ya bure leo.” Shosh wa watu sasa anaelekea kwamka tabasamu usoni- mababu wametuliza hasira. Kwa hivyo kofi hakulitarajia. Bare lilitua barabara usoni ama kama vile msomi anayeheshimika kijijini angesema the slap has reached ama the kofi has hit shosh vizuri. Msomi sasa anaheshimiwa na wanakijiji. Kizungu kilikuja na meli mwanakijiji aliyesikia hivyo angesema. Kilio kinatamalaki eneo. Jeshi ya boda linamshika Mjaka Mfine na kumvaa kofi. Mbona umpige kofi bikizee kama huyu??