Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Waziri wa Afya nchini, Ummy Mwalimu ameipa bodi mpya ya wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD)hadi ifikapo September 30 bohari hiyo iwe imebadilishwa kiutendaji na kurudishwa kwa mifumo ya tehama iliyosaidia kudhibiti mianya ya ubadhirifu ndani ya taasisi hiyo.
“Tumeondoa wale wakuu wa Idara lakini sasa badilisheni kama kuna mfanyakazi amekaa kitengo muda mrefu miaka mingi badilisheni. Hapa MSD mnaweza kusema ni mkurugenzi kumbe hata mtu wa chini anayepokea barua anafanya ubadhirifu. Sitaki tuingie tena kwenye masuala ya ubadhirifu”
Mnamo Mei 17, 2022 Wakurugenzi watano wa MSD waliondolewa kwenye nyadhifa zao kwa makosa ya ubadhirifu, yakiwemo yaliyotokana na Ripoti ya Mkaguzi Mkurugenzi wa Hesabu za Serikali (CAG)
Chanzo: Mwananchi