Serikali yaagiza TANESCO na Songas waanze kugawana mapato kwa usawa

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Waziri Medard Kalemani ameitaka Tanesco na Songas kuanza kugawana mapato kwa usawa kulingana na mkataba uliopo baina yao. Haya ndio maneno halisi ya waziri.

Ameeleza serikali na TFDL kwa ujumla wana hisa asilimia 36, lazima kuwe na usawa katikaugawaji wa mapato na TANESCO na Songas wanatakiwa wakae kwa pamoja waliangalie kimkataba

Waziri Kalemani aliyasema hayo alipokuwa akikagua mitambo ya ufuaji umeme ya Songas ambapo amekiri hakuna usawa kwenye mgawanyo wa mapato

Pia aliwaambia TANESCO wawe wanatoa taarifa kwa wananchi kipindi wanarekebisha mitambo yao ili kuepusha usumbufu wa umeme kukatika bila watu kuwa na taarifana wanapofanya marekebisho kwenye mtambo mmoja wasizime gridi nzima ya taifa

Jambo lingine amewataka TANESCO wawe na vifaa vya spare ndani ya nchi pindi vinavyoharibika na sio kuagiza nje ya nchi pindi tu vinapoharibika maana inachukua muda

Chanzo: Azam Tv
 
Mapato hapo anazungumzia "gross revenue" and "net profit"? Huwezi kugawana "revenue" kwa uwiano wa hisa na baadaye mwendeshaji aachiwe gharama za uendeshaji
 
Kumbe tanesco wanasubiri tatizo litokee ndiyo wanaagiza Spea, aisee kumbe hawana tofauti na bodaboda
 
Kwa kweli Tanesco wanatakiwa kubadilika
 
Back
Top Bottom