benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Moja kati ya masuala ambayo yamezoeleka kusumbua na kuleta tafrani katika jamii ya Watanzania ni uhaba wa Sukari ambao umekuwa ukitokea mara nyingi tu katika miaka iliyopita.
Katika kuhakikisha Watanzania wanasahau changamoto hiyo kwa kuhakikisha sukari inapatikana ya kutosha mwaka mzima Serikali imesema kuwa mwaka huu 2023 hakutakuwa na shida au uhaba wa Sukari huku ikiahidi kumaliza kabisa tatizo hilo ifikapo mwaka 2025/26.
Takwimu kutoka Bodi ya Sukari nchini zinaonesha kuwa uwezo wa kuzalisha Sukari nchini umeokua kwa kiasi kikubwa ambapo mwaka huu ni Tani 30,000 pekee zimeagizwa kutoka nje ya nchi kiasi ambacho ni zaidi ya nusu ya kiwango kilichoagizwa mwaka mmoja nyuma hali inayoonesha kuwa uwezo wa ndani wa kuzalisha na kusambaza sukari unazidi kukua siku baada ya siku.
Bodi ya Sukari ya Sukari imeeleza kuwa mazingira rafiki ya uwekezaji yaliyoletwa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan yamevutia uwekezaji zaidi katika Sekta ya Sukari ikiwemo wawekezaji wapya na wale waliokuwepo kupanua na kuongeza uzalishaji.
Uanzishwaji wa Kiwanda cha Bakhresa Sugar Limited umeongeza tani 18,000 kwenye mzunguko huku TPC ikiongeza tani 8,000, Kagera Sugar Ltd tani 10,000, Kilombero Sugar tani 8,000 (Kutoka tani 126,000 hasdi 134,000, huku uwekezaji unaofanywa ukitarajiwa kufikia tani 271,000 mwakani).
Pamoja na hivyo Kiwanda kipya cha Mkulazi kinachotarajiwa kuanza uzalishaji mwezi Juni kinatarajiwa kuzalisha tani 50,000, huku uwekezaji wa Mufindi Paper Mills Ltd wa Dola za Kimarekani Milioni 300 ukitarajiwa kuanza kuzalisha Sukari katika Wilaya ya Kasulu, Kigoma ifikapo 2025/26.
Wanajamvi, kama hii mipango isipokubwa na ufisadi na ubadhirifu uliokithiri katika "ishu" ya sukari basi nchi itakuwa imepiga hatua kubwa sana katika suala la uzalishaji na usambazaji wa sukari.