Serikali Yaahidi Kutatua Mgogoro wa Ardhi Kati ya Wananchi na Jeshi la Magereza Wilayani Ngara Mkoani Kagera

Serikali Yaahidi Kutatua Mgogoro wa Ardhi Kati ya Wananchi na Jeshi la Magereza Wilayani Ngara Mkoani Kagera

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

SERIKALI YAAHIDI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI KATI YA WANANCHI NA JESHI LA MAGEREZA WILAYANI NGARA MKOANI KAGERA

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imepokea malalamiko ya mgogoro wa Ardhi kati ya Wananchi na Jeshi la Magereza katika Kijiji cha Rusumo Wilayani Ngara Mkoani Kagera.

Kauli hiyo imetolewa Julai 30, 2024 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sillo wakati akizungumza na Wananchi wa kata ya Rusumo Wilayani Ngara Mkoani Kagera baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kutazama mgogoro uliopo baina ya Wananchi na Jeshi la Magereza.

Mhe. Sillo amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, nisikivu hivyo suala hilo la mgogoro huo atalifikisha katika vikao vya kamati ya maamuzi ili liweze kutatuliwa.

“Niwaombe wakazi wa kata na Kijiji hiki cha Rusumo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapenda sana na sisi kama Wizara tumewekwa kwa ajili ya kumuwakilisha yeye ili kutatua changamoto zenu, suala hili la Mgogoro huu nimelichukua na tutalishughulikia” Amesema Mhe. Sillo

Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba Ruhoro amesema kuwa, mgogoro huo umedumu kwa zaidi ya miaka 18 na kwamba umekuwa kikwazo katika utekelezaji wa shughuli za uzalishaji mali.

“Mhe. Naibu Waziri Mgogoro huu umedumu kwa zaidi ya miaka 18 sasa nikuombe utusaidie kwani wananchi wanakumbana na changamoto mbalimbali nakushindwa kufanya shughuli zao za uzalishaji mali ili kujiinua kiuchumi” Amesema Ruhoro.

Katika hatua nyingine Mhe. Sillo amesema Serikali ya Tanzania imetenga Dola milioni 100 kwa ajili ya kununua magari ya Zimamoto na Uokoaji hapa nchini ilikukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea.

“Eneo hili la Kituo cha forodha cha mpaka wa Rusumo ni eneo muhimu kwa ajili ya Uchumi wa Taifa letu na linahudumia nchini jirani ya Rwanda hivyo ni muhimu kuwa na vifaa vya utayari kwa ajili ya uokoaji pindi majanga yanapotokea” Amesema Mhe. Sillo

Kauli hiyo ameitoa baada ya kutembelea Kituo cha forodha cha mpaka wa Rusumo na kuambiwa na Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba kuwa katika eneo hilo kumekuwa kukitokea ajali za Malori kuwaka moto lakini hakuna gari

Screenshot 2024-07-31 at 11-09-28 nick media (@nickmediatz) • Instagram photos and videos.png
Screenshot 2024-07-31 at 11-09-42 nick media (@nickmediatz) • Instagram photos and videos.png

Screenshot 2024-07-31 at 11-10-15 nick media (@nickmediatz) • Instagram photos and videos.png
 
Back
Top Bottom