Serikali yaahidi kuunganisha umeme Afrika

Serikali yaahidi kuunganisha umeme Afrika

mwakani naolewa

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
148
Reaction score
426
Serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania yaahidi kuunganisha bara la Afrika kwa nishati ya umeme kupitia mradi mkubwa wa usafirishaji umeme unaohusisha ujenzi wa njia za usafirishajiumeme wa msongo wenye kilovoti 400 kutoka iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha Tanzania na Zambia {TAZA} pamoja na vituo vya kupoza umeme vya Tagameza, Kisada, Iganjo, Nkemango na Malangalali.

Ameyasema hayo Naibu Waziri mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Doto Biteko huko Sumbawanga mkoani Rukwa akiweka jiwe la msingi la utekelezaji wa mradi huo kutoka Tunduma hadi Nakonde mpakani mwa Tanzania na Zambia

Aidha Waziri Biteko ametaja miradi mingine inayotekelezwa kua ni umeme wa jua Kishapu(MW150), Malagarasi(MW49.5) na mradi wa gesi asilia lengo likiwa ni kupata umeme wa uhakika.

IMG_2492.jpeg
IMG_2493.jpeg
IMG_2494.jpeg
IMG_2491.jpeg
 
Back
Top Bottom