Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Yah: KUAHIRISHA UTEKELEZAJI WA MTAALA ULIOBORESHWA WA KIDATO CHA TANO MWAKA WA MASOMO 2024/2025
Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) ilipokea barua yenye Kumb. Na DC.297/507/01/370 ya tarehe 09/7/2024 kutoka OR-TAMISEMI kuhusu changamoto zilizopo katika utekelezaji wa Mtaala Ulioboreshwa wa Kidato cha Tano ulioanza kutekelezwa tarehe 01/07/2024 na kushauri kwamba utekelezaji huo uahirishwe ili uanze mwaka 2025. Aidha, taarifa ya kikaokazi cha pamoja kati ya WyEST na OR-TAMISEMI kilinaini kuwa chnangamoto zilizopo ni ukosefu wa nakala ngumu za vitabu kwa matumizi ya wanafunzi na walimu na utoaji wa mafunzo kabilishi kwa walimu.
Kufuatilia ombi hilo, WyEST kupitia barua yenye Kumb. Na. AC. 128/191/01D/99 ya tarehe 22/7/2024 kwenda Ofisi ya Rais – TAMISEMI iliridhia kuahirishwa kwa utekelezaji wa Mtaala Ulioboreshwa wa Kidato cha Tano kwa mwaka 2024 ili uanze kutekelezwa mwaka 2025 baada ya changamoto hizo kutatuliwa.
Hivyo, WyEST inashauri kwamba, utekelezaji wa mtaala husika kwa upande wa Zanzibar uahirishwe kwa sababu utahini wa wanafunzi wa Sekondari ya juu (A-Level) kati Tanzania Bara na Zanzibar hutumia mtihani mmoja
Nashukuru kwa ushirikiano wako
Pro. Carolyne I. Nombo
KATIBU MKUU
Pro. Carolyne I. Nombo
KATIBU MKUU
Pia soma