Serikali yaanza mchakato wa viwanda vya simu janja

Serikali yaanza mchakato wa viwanda vya simu janja

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeanza mchakato wa uanzishwaji wa viwanda vya utengenezaji wa simu janja ndani ya nchi vitakavyowezesha upatikanaji rahisi wa vifaa hiyo.

Waziri Dk Faustine Ndugulile alisema hayo jana wakati wa kikao kazi na wenyeviti wa bodi na wakuu wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.

Alisema utaratibu umeshaanza na kiwanda kimojawapo kinatarajiwa kujengwa Mwanza wananchi wamudu kununua simu hizo nchini.

“Ilani ya CCM imetaka tuongeze wigo wa mawasiliano na kuongeza matumizi ya intaneti, hatutaweza kufanikiwa kama wananchi hawatamudu kununua simu janja. Na sisi tumeliona hilo na ndio maana tumeanza mchakato wa kuanzisha viwanda vyetu ndani ya nchi ambavyo vitaanza kutengeneza simu janja," alisema Dk Ndugulile.

Alisema kiwanda kitakachojengwa Mwanza kitakuwa kinazalisha simu na kuziunza kwa Watanzania kwa bei nafuu.

“Nitoe rai kwa Watanzania, mwekezaji yeyote mwenye nia ya kuwekeza kwenye Tehama aje kwenye wizara yetu na tutampa ushirikiano asilimia 100 kuhakikisha kwamba tunatengeneza bidhaa ambazo zitatumika ndani ya nchi ili wananchi wapate simu janja kwa gharama nafuu,” alisema.

Alisema duniani pamoja na kuwapo janga la corona kampuni zilizofanya vizuri na kupata faida kubwa zilikuwa ni za mitandao na kwamba Tanzania kwa sasa inapiga hatua.

“Tuna vijana wabunifu, hakodi fremu kwa ajili ya biashara anaagiza biashara yake nje ya nchi, anafikisha nchini anaweka nyumbani anapiga picha na kutangaza mitandaoni na anauza kupitia mtandao na kukufikishia mzigo wako nyumbani,” alisema.

Wakati huo huo, Dk Ndugulile aliwataka wenyeviti wa bodi na wakuu wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kusimamia kudhibiti ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za taasisi zao.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Zainab Chaula alimhakikishia waziri kuwa aliyoagiza katika kikao kazi hicho yatatekelezwa kufikia maono ya Rais John Magufuli, ya kupanua wigo wa mawasiliano na matumizi ya intaneti.

Chanzo: Habari Leo
 
Aisee niwe tu mkweli izo simu zinazo tengenezwa na serikali hazitakua na unafuu wowote

Tupo tuombe uzima.
 
Kumbe na huyu ni mchumia tumbo/muimba mapambio kama wapuuzi wengine!
 
Ndugulile anasema anataka internet iwe kubwa na mawasiliano huku wao wakizima twitter,tunasafari ndefu sana
 
Ndugulile anasema anataka internet iwe kubwa na mawasiliano huku wao wakizima twitter,tunasafari ndefu sana
102011131.jpg
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Waziri apambane gharama za kupiga na kupokea simu na vifurushi viwe rafiki.
 
Aliahidi kutusaidia kushusha gharama za matumizi, halijaisha, anakuja na ujenzi wa viwanda vya simu! Anaweweseka tu huyu naye! Chini ya pombe kofuri, viongozi akili zinabuma!!
 
Aliahidi kutusaidia kushusha gharama za matumizi, halijaisha, anakuja na ujenzi wa viwanda vya simu! Anaweweseka tu huyu naye! Chini ya pombe kofuri, viongozi akili zinabuma!!
Anajua tumeshasahau.
 
Back
Top Bottom