Serikali Yabainisha Mikakati ya Kurejesha Hadhi ya Madini ya Tanzanite

Serikali Yabainisha Mikakati ya Kurejesha Hadhi ya Madini ya Tanzanite

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

SERIKALI YABAINISHA MIKAKATI YA KUREJESHA HADHI YA MADINI YA TANZANITE

-Waziri Mavunde azindua mnada wa ndani Mirerani.

- Minada ya ndani na nje ya nchi kutumika kutangaza madini ya vito.

-Madini yote yatakayokosa wanunuzi kurejeshwa kwa wahusika

-Wadau waonesha nia ya kujenga Mji wa Kimadini Mirerani

Mirerani

MANYARA: Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema Serikali imejidhatiti kurudisha hadhi ya Tanzanite kwa kufanya minada ndani na nje ya nchi ili kuyaongezea thamani na wafanyabiashara waweze kunufaika na kuongeza pato la taifa kwa ujumla.

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameyasema hayo Desemba 14, 2024 Mirerani mkoani Manyara wakati akizindua mnada wa madini ya vito ambao mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2017.

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema mojawapo ya maeneo yanayosaidia kuongeza mapato ni pamoja na kudhibiti biashara ya madini, kuzuia utoroshaji na kuifanya biashara hiyo kuwa katika mfumo sahihi, uwepo wa minada utachochea uongezaji thamani ya madini ya vito.

“Madini ya Vito yananunuliwa kwa asilimia kubwa kwa ajili ya ‘luxury’ ni ufahari na madini ya vito tunashindana na watu wengine ndio maana Serikali inaendelea kuchukua hatua, tunarudisha hadhi ya Tanzanite ili ikashindane vizuri duniani" Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde

“Moja ya hatua ya kwanza ni urejeshaji wa minada ya ndani na ya kimataifa, ili tuyape thamani madini yetu, duniani kuna madini mengi ya vito, moja ya sifa kubwa ya madini ya vito ni uadimu, Tanzanite ina sifa hizo; Ila sio madini pekee yake adimu, kuna nchi nyingine zina madini adimu ambayo hayapatikani popote hivyo tunashindana kimataifa ni lazima tuchukue hatua kuhakikisha tunarudisha hadhi ya Tanzanite katika soko la kimataifa ili na bei iweze kuongezeka na wafanyabiashara wanufaike" Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde Amesema, katika vipengele (category) vya mawe duniani, jiwe linaanzia kuwa Precious, semi-Precious halafu baadaye linakuwa jiwe la kawaida na kwamba wanachukua hatua za makusudi ili Tanzanite lisiwe jiwe la kawaida.

“Tukiacha liwe la kawaida mtanunua kwa kilo kwa gharama ndogo sana na mtashusha hadhi ya Tanzanite, Serikali haipo tayari kuona hilo linatokea" Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde

"Kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Manyara, nimeishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada zilizofanyika kurejesha huduma hii ya uuzaji wa madini ya vito kwa njia ya Mnada. Kurejeshwa kwa minada ya aina hii ni kusudio la Serikali katika kuhakikisha rasilimali za madini zinawanufaisha kiuchumi Watanzania wote" RC Manyara, Mhe. Queen Sendiga

"Serikali katika kuboresha eneo la machimbo ya Tanzanite itajenga Zahanati kwa gharama ya Shilingi Milioni 250 yenye hadhi ya kituo cha Afya ndani ya eneo la Ukuta ili kusaidia wagonjwa wa kawaida na wale wanaopatwa na ajali migodini." RC Manyara, Mhe. Queen Sendiga
 

Attachments

  • Gexcx6dWMAErqDw.jpg
    Gexcx6dWMAErqDw.jpg
    418.6 KB · Views: 3
  • Gexcx6bXYAAI02t.jpg
    Gexcx6bXYAAI02t.jpg
    455.7 KB · Views: 4
  • Gexcx6bXcAAaEFl.jpg
    Gexcx6bXcAAaEFl.jpg
    387.7 KB · Views: 3
  • Gexcx6WWQAAZDEQ.jpg
    Gexcx6WWQAAZDEQ.jpg
    241.6 KB · Views: 3
  • GewtGpEWcAA7v6T.jpg
    GewtGpEWcAA7v6T.jpg
    368.3 KB · Views: 2
  • GewtGtsW0AAKKIi.jpg
    GewtGtsW0AAKKIi.jpg
    373.8 KB · Views: 4
  • GewttPyXAAEXEju.jpg
    GewttPyXAAEXEju.jpg
    61.7 KB · Views: 6
  • GewtthKXwAAlNog.jpg
    GewtthKXwAAlNog.jpg
    544.1 KB · Views: 3
  • Ges2-8QWkAI-Rag.jpg
    Ges2-8QWkAI-Rag.jpg
    300.8 KB · Views: 3
  • GewEH86XoAAierE.jpg
    GewEH86XoAAierE.jpg
    59.4 KB · Views: 3
  • Ges2-8OXwAAw2Kt.jpg
    Ges2-8OXwAAw2Kt.jpg
    340.6 KB · Views: 4
  • Ges2-9tXUAAQRlk.jpg
    Ges2-9tXUAAQRlk.jpg
    345.1 KB · Views: 3
  • GeuDa5hXcAER24a.jpg
    GeuDa5hXcAER24a.jpg
    375.5 KB · Views: 4
  • GeuDa3zW8AEhyXS.jpg
    GeuDa3zW8AEhyXS.jpg
    438.2 KB · Views: 3
  • GeuDa4-X0AAEdGy.jpg
    GeuDa4-X0AAEdGy.jpg
    255.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom