Donnie Charlie
JF-Expert Member
- Sep 16, 2009
- 16,908
- 19,123
Dar es Salaam. Serikali imefafanua kuhusu kupinda kwa daraja la juu la makutano ya barabara za Nyerere na Kawawa eneo la taa za Veta - Chang'ombe ikisema limejengwa hivyo kutokana na usanifu wake.
Akizungumza leo Novemba 15 wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Meneja wa ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo haraka wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Barakael Mmari amesema kumekuwa na maneno kwamba daraja hilo limepinda na haliko katika viwango vinavyohitajika.
Ameendelea kusema kuwa, daraja hilo halionekani limenyooka moja kwa moja kama yaliyo mengine kutokana na usanifu uliobuniwa.
"Hili limesanifiwa hivi kwa sababu maalumu, daraja lina njia mbili na limejengwa katika maeneo mawili tofauti na upande wa katikati itajengwa barabara ya mabasi ya mwendokasi.
"Upande wa kushoto kama unaelekea uwanja wa ndege ni magari yanatoka mjini kuelekea huko na upande wa kulia ni magari yanayotoka uwanja wa ndege kwenda mjini," amesema Mmari.
Amesema pia kutakuwa na mabasi yanayotoka moja kwa moja uwanja wa ndege kwenda mjini na kutoka mjini kwenda uelekeo wa uwanja wa ndege.
Pia amesema kutakuwa na mabasi yanayotoka uwanja wa ndege kwenda Chang' ombe au Magomeni.
"Kwa maana hiyo hapa katika daraja limekuja na njia mbili ili kupata magari yanayokwenda kushoto na kulia, tumetengeneza njia za ziada zitakazosaidia kuwezesha mpishano wa magari yanayokwenda kushoto na kulia.
"Huu mpindo unaonekana umefanywa hivyo ili kupata nafasi pale chini na kuleta ufanisi wa mabasi yatakayopita," amesema Mmari.
Akizungumzia sula hilo, Waziri Mbarawa amesema, "Kuna mtu ameandika limepinda limepinda... Mambo ya kitaalamu yanakwenda kitalaamu, daraja halijapinda isipokuwa usanifu maalumu umetengenezwa ili kuwezesha njia nyingine za mabasi," amesema Profesa Mbarawa.
Mwanainchi.