Serikali yafafanua madereva kuzuiwa kuingia Zambia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu Idara ya Uhamiaji nchini Zambia kuwazuia madereva wa IT katika mpaka wa Tunduma Mkoani Songwe kuingia nchini Zambia, ikiwa ni katika kujikinga na Virusi vya Corona.
boda1.jpg

Kituo cha ukaguzi mpakani mwa Tanzania na Zambia
Mkuu wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe, Juma Said Irando ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, ametolea ufafanuzi wa malalamiko ya madereva hao wa IT waliokwama mpakani kwa takribani wiki mbili sasa.

"Mpaka wa Tunduma unahudumia nchi mbili, watumiaji wa mpaka huu wafuate utaratibu unaotakiwa kulingana na sheria za nchi zote mbili, Tanzania ina sheria zake na wale wanaokwenda nchi ya pili kule wafuate sheria zake" amesema Mkuu huyo wa Wilaya.

"Tukifuata sheria za nchi zote mbili tutaishi kwa wema na amani na kudumisha mahusiano yetu yaliyodumu kwa muda mrefu sasa", ameongeza.

Awali madreva hao waliiomba serikali ya Tanzania kuingilia suala hilo ili kumaliza utata wa changamoto wanazokutana nazo .

Aidha uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) umesema, utatoa muongozo kuhusu msamaha wa faini kwa madereva watakaokaa karantini siku 14 wakati nyaraka zikiwataka kuvuka mpakani ndani ya siku 7 ili kuondoa usumbufu.

Chanzo: EATV

Wanataka rushwa pia. Wanautumia mwanya. Sasa hao wanaoshushwa kwenye mabasi si tayari wameshausambaza? Na ukitoa kwacha 300 ndo unakuwa huna corona!🤦🏾‍♂️
 
Ila Corona inachotufanyia! Ni Mungu tu ndiye ajuaye.
 
Kwasababu Serikali yetu haichukui hatua zozote dhidi corona naona majirani zetu wanaona kuwa Watanzania kwa sasa wote wana colona
Sasa nchi imeshakuwa kama Ecuador, maiti zinaokotwa mitaani Mkuu..
Nchi zote majirani zinaiogopa Tz kwa corona..
Jamaa limejifungia Chato tu.
 
Waendelee tu kujifungia na kufafanua alafu pia wafafanue madereva watz wanaokutwa na Corona wakitokea tz huko Kenya Uganda Burundi etc
 
Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu Idara ya Uhamiaji nchini Zambia kuwazuia madereva wa IT katika mpaka wa Tunduma Mkoani Songwe kuingia nchini Zambia, ikiwa ni katika kujikinga na Virusi vya Corona.
boda1.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe, Juma Said Irando ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, ametolea ufafanuzi wa malalamiko ya madereva hao wa IT waliokwama mpakani kwa takribani wiki mbili sasa.

"Mpaka wa Tunduma unahudumia nchi mbili, watumiaji wa mpaka huu wafuate utaratibu unaotakiwa kulingana na sheria za nchi zote mbili, Tanzania ina sheria zake na wale wanaokwenda nchi ya pili kule wafuate sheria zake" amesema Mkuu huyo wa Wilaya.

"Tukifuata sheria za nchi zote mbili tutaishi kwa wema na amani na kudumisha mahusiano yetu yaliyodumu kwa muda mrefu sasa", ameongeza.

Awali madreva hao waliiomba serikali ya Tanzania kuingilia suala hilo ili kumaliza utata wa changamoto wanazokutana nazo .

Aidha uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) umesema, utatoa muongozo kuhusu msamaha wa faini kwa madereva watakaokaa karantini siku 14 wakati nyaraka zikiwataka kuvuka mpakani ndani ya siku 7 ili kuondoa usumbufu.

Chanzo: EATV

View attachment 1432291
Poleni sana ndugu zetu.
 
Hii taarifa sijaielewa. Wamekatazwa kuingia au wametakiwa kukaa karantini siku 14.

Taarifa kama hizi zinazikuwa na ujumbe unao-hang ndio tatizo lenyewe kuliko tatizo linaloripotiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom