Serikali yafunga Mtambo Wa Kuchakata Asali Wilayani Manyoni

mamayoyo1

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
1,011
Reaction score
1,019

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umefunga mtambo wa kuchakata asali wilayani Manyoni mkoani Singida.

Akizungumza jana Machi 14,2019 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TFS Tulizo Kilaga amesema mtambo huo wa kisasa una uwezo wa kuchakata lita 500 kwa siku.

Amesema kuwa mtambo huo umegharimu Sh.milioni 80 na unatarajiwa kuondoa changamoto ya uwepo wa asali yenye kiwango duni cha ubora katika ukanda huo na maeneo maeneo ya jirani.

“Mtambo huu umefungwa katika kiwanda cha TFS na utatumiwa na wafugaji wa nyuki wa ndani pamoja na nje wote wataruhusiwa kuchakata mazao yao,”amesema Kilaga.

Ameongeza kuwa kiwanda hiko kwa kiasi kikubwa kitategemea mali ghafi toka kwenye msitu wa Aghondi uliopo eneo la Itigi na uwepo wa mtambo huo pia utasaidia kutunza mazingira kwani watakuwa na uhakika wa soko la asali yao.
Pia amesema katika uvunaji wa awali wamefanikiwa kuvuna mizinga 459 kati ya 729 na kupata asali kilo 6,175 sawa na tani 6.175 wastani kilo 13.45 kwa mzinga.
Akizungumzia mtambo huo, Meneja wa TFS wilayani Manyoni Juma Mambo amesema utasaidia kupatikana kwa asali bora na hivyo kuwa na uhakika wa soko la ndani na nje ambalo litawafanya wadau
 
Hii habari ni njema sana, lakini haijapewa publicity inayostahili kama vitu vingine vidogo vidogo vinavyokuzwa sana. Kuna jambo halijawekwa sawa hapa ni kuwa naona ubora wa asali hii unaweza ukawa unaongoza Tanzania kwa kuwa Itigi haina Tumbaku sana na hivyo asali yake with that processing ikawa ni export material. Sasa mnyororo wa solo haujaelezwa umeandaliwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…