Serikali yaipa kongole Multichoice kutangaza Kombe la Dunia kwa Kiswahili

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeipongeza kampuni ya Multichoice kupitia DStv kuamua kutangaza kwa Kiswahili Mashindano ya Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu nchini Qatar.

Akizungumza Septemba 01, 2022 Dar es Salaam katika hafla ya Maonesho kwa Vyombo vya Habari ya kampuni hiyo, kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Mohamed Mchengerwa, Naibu Katibu Mkuu Saidi Yakubu ameipongeza DStv kwa kuendelea kuunga mkono maendeleo ya sekta ya sanaa na michezo nchini.

Nitumie nafasi hii kuwapongeza DStv, kwa kutambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili na kuamua kutangaza mechi 64 za Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2022 kwa lugha hiyo, ili Watanzania wengi waburidike kupitia lugha yao," amesema Ndugu Saidi Yakubu.

Amesema DStv imeendelea kuonesha dunia maudhui ya kitanzania kupitia filamu zinazooneshwa chanel ya Maisha Magic Bongo na Maisha Magic Poa ambayo imesaidia watanzania kuonesha vipaji na kupata kipato.

Ameongeza kuwa, kampuni hiyo imekua Mdau mkubwa wa wizara katika hasa katika kipindi hichi ambacho sekta zake zimekua na ubunifu ambao umeleta tija kwa taifa.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu Yakubu, ameishukuru kampuni hiyo, kwa kuanzisha programu za kusaka vipaji katika tasnia ya filamu, sambamba na kutoa ajira kwa watanzania.

Amesema kuwa, soko la filamu za kitanzania limepanuka na limeingia katika ushindani wa Kimataifa, ikiwemo katika Tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards, ZIKOMO na Zanzibar International Film Festival.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa, changamoto ya Hakimiliki katika kazi za ubunifu imeendelea kufanyiwa kazi, ambapo hivi karibuni Mhe. Waziri aliunda kamati ya kushughulikia kero hiyo ambayo tayari imewasilisha mapendekezo na Serikali inayafanyia kazi.
 
Attachments

  • IMG-20220901-WA0217.jpg
    IMG-20220901-WA0217.jpg
    82.5 KB · Views: 7
  • IMG-20220901-WA0218.jpg
    IMG-20220901-WA0218.jpg
    120 KB · Views: 7
  • IMG-20220901-WA0231.jpg
    IMG-20220901-WA0231.jpg
    120.4 KB · Views: 7
  • IMG-20220901-WA0212.jpg
    IMG-20220901-WA0212.jpg
    52.2 KB · Views: 7
  • IMG-20220901-WA0224.jpg
    IMG-20220901-WA0224.jpg
    52.7 KB · Views: 6
  • IMG-20220901-WA0229.jpg
    IMG-20220901-WA0229.jpg
    63.3 KB · Views: 7
  • IMG-20220901-WA0213.jpg
    IMG-20220901-WA0213.jpg
    92.9 KB · Views: 9
  • IMG-20220901-WA0214.jpg
    IMG-20220901-WA0214.jpg
    93 KB · Views: 9
  • IMG-20220901-WA0222.jpg
    IMG-20220901-WA0222.jpg
    73.4 KB · Views: 9
  • IMG-20220901-WA0227.jpg
    IMG-20220901-WA0227.jpg
    90.4 KB · Views: 8
  • IMG-20220901-WA0232.jpg
    IMG-20220901-WA0232.jpg
    104.1 KB · Views: 9
  • IMG-20220901-WA0228.jpg
    IMG-20220901-WA0228.jpg
    97.1 KB · Views: 8
Hiyo mbona kitambo Sana!?

Tangu zamani wanafanya Hivyo!!

Hata euro ilikuwa Hivyo Hivyo hata KOMBE la Dunia lililopita pita pia!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"!
 
Kombe la Dunia ilitakiwa Tanza-nia iwe na channel yake dedicated kabisa hii inasaidia kukuza interest ya michezo kwa Vijana na sio kuwategemea DSTV ambao watapandisha Bei na kufanya Watanzania Wachache kufaidi
 
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeipongeza kampuni ya Multichoice kupitia DStv kuamua kutangaza kwa Kiswahili Mashindano ya Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu nchini Qatar.

Akizungumza Septemba 01, 2022 Dar es Salaam katika hafla ya Maonesho kwa Vyombo vya Habari ya kampuni hiyo, kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Mohamed Mchengerwa, Naibu Katibu Mkuu Saidi Yakubu ameipongeza DStv kwa kuendelea kuunga mkono maendeleo ya sekta ya sanaa na michezo nchini.

Nitumie nafasi hii kuwapongeza DStv, kwa kutambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili na kuamua kutangaza mechi 64 za Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2022 kwa lugha hiyo, ili Watanzania wengi waburidike kupitia lugha yao," amesema Ndugu Saidi Yakubu.

Amesema DStv imeendelea kuonesha dunia maudhui ya kitanzania kupitia filamu zinazooneshwa chanel ya Maisha Magic Bongo na Maisha Magic Poa ambayo imesaidia watanzania kuonesha vipaji na kupata kipato.

Ameongeza kuwa, kampuni hiyo imekua Mdau mkubwa wa wizara katika hasa katika kipindi hichi ambacho sekta zake zimekua na ubunifu ambao umeleta tija kwa taifa.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu Yakubu, ameishukuru kampuni hiyo, kwa kuanzisha programu za kusaka vipaji katika tasnia ya filamu, sambamba na kutoa ajira kwa watanzania.

Amesema kuwa, soko la filamu za kitanzania limepanuka na limeingia katika ushindani wa Kimataifa, ikiwemo katika Tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards, ZIKOMO na Zanzibar International Film Festival.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa, changamoto ya Hakimiliki katika kazi za ubunifu imeendelea kufanyiwa kazi, ambapo hivi karibuni Mhe. Waziri aliunda kamati ya kushughulikia kero hiyo ambayo tayari imewasilisha mapendekezo na Serikali inayafanyia kazi.
Hili ni Tangazo la biashara

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom