Serikali yaipa NHIF miezi mitatu kuimarisha mfumo wa TEHAMA kuondoa usumbufu wa wagonjwa wa Bima

Serikali yaipa NHIF miezi mitatu kuimarisha mfumo wa TEHAMA kuondoa usumbufu wa wagonjwa wa Bima

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Geita Mjini, Constantine John Kanyasu (Kwa niaba ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu) aliyeuliza kwa nini NHIF inazuia matibabu ya baadhi ya wagonjwa wenye Bima za Afya wakiwa Hospitali.

“Ni kweli kulikuwa na zoezi la uhakiki wa uhalali wa wanufaika wa mfuko wa bima ya Afya, zoezi hilo lilileta usumbufu ambao ungeweza kuzuilika kama wahakiki hao wangetumika wataalamu wenye miiko ya taaluma ya tiba,” Dkt. Godwin Mollel.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, ameitaka Menejimenti ya Mfuko wa Bima ya Afya katika kipindi cha miezi mitatu ihakikishe inaboresha mifumo ya TEHAMA itakayoweza kuondoa usumbufu na pia kudhibiti udanganyifu pasipo kuwa kero kwa wanufaika wa Mfuko.

Pia Dkt. Mollel, amesema Serikali ilipopata malalamiko hayo ilifuatilia mara moja na kufanya maboresho ambayo yaliyoondoa usumbufu kwa wateja na wateja kuendelea kupata Huduma kwa ufasaha.

Baada ya kulidhishwa na majibu ya Naibu waziri wa Afya, Mbunge wa Geita Mjini, Constantine John Kanyasu, amempongeza na kufurahishwa majibu yalitolewa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel.

Pia soma hoja ya memba kuhusu changamoto hiyo - NHIF imeikosesha nchi utawala wa sheria
 
Nchi ya kishenzi, kwa hiyo miezi mitatu watu wasumbuke na wafe?
 
Nsibu waziri ni dactari kweli?anapwaya Sana.
 
TOTO afya kadi waliondoa, halafu Hakuna alternative.

Hawakufanya maandalizi ya hicho wanachosema kuwa watoto wakate shuleni. Je, waliandaa utaratibu, ili kwanza watoto wapate Bima ndio waondoe TOTO Bima NHIF?
 
Miezi 3 yote hiyo,hii nchi kweli haiko serious

Ova
 
Bima Bhana. Sasa kwann mnatoa bima za afya znazokwisha muda wake?
 
Back
Top Bottom