Serikali yairuhusu Yanga kutumia Uwanja wa Taifa

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411



Serikali imesaini Mkataba na Klabu ya Yanga kutumia Uwanja Mkuu wa Taifa pamoja na Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya michezo yote ya Kimataifa pamoja na michezo ya Ligi Kuu ya ndani.

Mkataba huo umesainiwa jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Serikali na Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Baraka Deusdedit kwa niaba ya Klabu ya Yanga.

Katika Mkataba huo, Klabu ya Yanga imeruhusiwa kutumia viwanja hivyo kama viwanja vyake vya nyumbani kwa sharti la kuvitunza viwanja hivyo wakati wote wanapovitumia.

Miongoni mwa masharti hayo ni kutunza viwanja, mali na vifaa vyote vilivyopo katika viwanja hivyo, na endapo kutatokea uharibifu wowote utakaofanywa na wachezaji ama mashabiki, Klabu hiyo itawajibika kubeba gharama za matengenezo yote yatakayotokana na uharibifu huo.

Aidha, Klabu ya Yanga inaweza kutumia viwanja hivyo kwa mazoezi ya kujianadaa na mechi zinazowakabili.

Chanzo: Dewji
 
Sasa jamaa zangu wa ule mtaa karibu na pombe shop ya zamani msijetufanyia inda kwa kuharibu viti na mageti ya uwanjani baada ya kuchukua kichapo kwenye mechi ya marudiano mbele ya refa toka ujerumani. Huu ni utani tuu jamani
 
Kufanyia mazoezi?
Hapo lazima tff iingilie
Mkuu, mwenye uwanja ni serikali sio TFF. Wao wanapewa taarifa tu kuwa uwanja wa nyumbani ni upi
Malinzi ajenge uwanja wa TFF. Matokeo yake kaenda kuboresha kwa Kaitaba
 
Kuna kitu Bado sijaelewa
  • Yanga wamekodishiwa au!
  • Ni ipi Gharama ya Mkataba?
  • Nini tofauti ya Sasa na Mwanzo Kabla ya Kufungiwa?
  • Simba, nao wanahitaji Mkataba kutumia Uwanja au bado kuruhusiwa?
 
Kuna kitu Bado sijaelewa
  • Yanga wamekodishiwa au!
  • Ni ipi Gharama ya Mkataba?
  • Nini tofauti ya Sasa na Mwanzo Kabla ya Kufungiwa?
  • Simba, nao wanahitaji Mkataba kutumia Uwanja au bado kuruhusiwa?
Simba wanashiriki mashindano ya aina gani?kama ni mapinduzi cup hua inafanyikia zanzibar kwa nnanvyojua
 
Yanga janja sana,imewahi hiyo ili kule CAF vile vipengere timu mwanachama lzm iwe na viwanja vya mechi/mazoezi isiwakumbe? ( nawaza)
 
Ni aibu kwa vilabu vyetu vikongwe kukosa viwanja mpaka muda huu....

Hii inaleta tafsiri nyingi mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…