Serikali yajipanga kuongeza walipa kodi

Serikali yajipanga kuongeza walipa kodi

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
119
Reaction score
240
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha sekta binafsi inayoiwezesha nchi kukuza uchumi na kupata maendelo.

Dk Mwigulu aliwaeleza washirika wa kongamano la kodi Dar es Salaam jana kuwa watanzania wanatakiwa kutafakari uhusiano uliopo kati ya kodi na maendeleo ya taifa kwa sababu kuna kulegalega katika kukubali kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kodi na maendeleo ya nchi.

Dk Mwigulu anasema ujenzi wa barabara, madarasa, kituo cha afya, mbolea, maji au umeme au kitu chochote kinachohusiana na masuala ya maendeleo kina uhusiano wa moja kwa moja na kodi na kwamba hata nchi ikikopeshwa marejesho yake yataangalia kodi.

Yoyote atakayeanzisha shughuli za uzalishaji, watendaji wote serikalini wanatakiwa wamkimbilie baada ya kumkatisha tamaa. Watu milioni moja wanaingia kwenye soko la ajira kila mwaka kutoka shuleni na vyuoni hivyo Taifa linahitaji sekta binafsi imara ili kuongeza wigo wa walipa kodi.

7Mf0vuBl01nDRwWy
 
Ndiyo huyu aliyesema kuna walipa kodi milioni 3 tu kati ya Watanzania milioni 62!! Ok.

Yaani kodi tozo kwenye mafuta na miamala ya simu, kodi ya majengo kwenye mita za LUKU kila mwezi, nk. Zote hizo zinawagusa watu miliooni 3 pekee!! Ok.

Kila la heri kwake.
 
Back
Top Bottom