Serikali yakabidhi gari la kubebea wagonjwa, litatoa huduma kwa wafungwa na mahabusu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Senga Gugu leo amezindua na kukabidhi jumla ya magari 11 huku gari moja likiwa ni Gari la Kubebea Wagonjwa ambapo pia gari hilo litataoa huduma kwa wafungwa na mahabusu katika gereza la Ukonga na Magereza ya karibu.
Katibu Mkuu amezindua na kukabidhi magari hayo Oktoba 2, 2024 katika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Msalato jijini Dodoma huku akiwasihi vyombo hivyo vikaongeze ufanisi katika shughuli mbalimbali za magereza na urakibu.
Magari hayo yana gharama ya Shilingi Za Kitanzania Bilioni 2.25.