Serikali yakamilisha ujenzi wa daraja linalounganisha Halmashauri ya Buchosa na Kijiji cha Lubanga, Wilaya ya Geita

Serikali yakamilisha ujenzi wa daraja linalounganisha Halmashauri ya Buchosa na Kijiji cha Lubanga, Wilaya ya Geita

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Wananchi wa Buchosa na Geita hatimaye wameondokana na kero ya usafiri baada ya ujenzi wa daraja linalounganisha Halmashauri ya Buchosa na Kijiji cha Lubanga, Wilaya ya Geita kukamilika.

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, amesema daraja hilo lilikuwa moja ya changamoto kubwa aliyokuwa akiitafutia suluhisho tangu alipochaguliwa, kwani wananchi walikuwa wakipata adha kubwa kuvuka, hasa wakati wa mvua.

Kabla ya daraja hilo kujengwa, baadhi ya wafanyabiashara walijenga daraja la miti na kuwalazimisha wananchi kulipa Shilingi 1,000 ili kuvuka kutoka Buchosa kwenda Geita na kinyume chake. Shigongo anasema hali hii ilikuwa mzigo mkubwa kwa wananchi, hususan wakulima na wafanyabiashara wadogo, hivyo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza kilio cha Wanabuchosa na kuhakikisha daraja hili linajengwa.

Diwani wa Kata ya Nyanzenda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa, Idama Kibanzi, amesema kuwa juhudi za Mbunge Shigongo zilichangia pakubwa kuhakikisha daraja hilo linajengwa.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Buswelu wamepongeza juhudi za Mbunge Eric Shigongo na Rais Samia, wakisema kuwa maendeleo yanayoonekana ni ushahidi wa uongozi bora.

Daraja hili si tu limeboresha usafiri kati ya Buchosa na Geita, bali pia limechochea ukuaji wa biashara na uchumi wa wananchi, huku likirahisisha upatikanaji wa huduma muhimu kama afya na elimu.
 
Back
Top Bottom