Serikali yakanusha kukamatwa kwa Mwandishi Dickson Ng'hily na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, yasema mwandishi hakupigwa wala kuvunjiwa simu yake

Serikali yakanusha kukamatwa kwa Mwandishi Dickson Ng'hily na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, yasema mwandishi hakupigwa wala kuvunjiwa simu yake

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Haya maelezo yanatishia mashaka, kwamba wanafunzi hawakai chini ila walikuwa wanafanya masahihisho ya mitihani, tena chini ya mti, kama vyumba vinawatosha kwanini wasifanyie hayo darasani? Hapa panatia mashaka.

Ila pia mnataka kutuambia kuwa THRDC walikurupuka, kwamba hawakuwa na taarifa sahihi hawakaja tululisha kachumbari huku?

Lakini pia historia inawaangusha, si tulishuhudia mlivyohenyesha mwandishi wa habari wa habari aliyepiga picha kwenye shule iliyopo Mbeya, ambao nao walikuwa wakikaa chini, kama sikosei jambo lilifika mpaka kwa Waziri Mkuu?

Kama stori hiyo ilikupita soma hapa:

- Mbeya: Mwalimu aliyesambaza picha za Wanafunzi wamekaa chini, aingia matatani

- Mwalimu wa field aliyesambaza picha za watoto wamekaa chini kufukuzwa (uhaba wa madawati)

Halafu mnatupanga hapa kwamba mko open kuwaacha waandishi wa habari wafanye kazi yao bila bugudha?

=====

KUKANUSHA TAARIFA YA KUKAMATWA KWA MWANDISHI DICKSON NG’HILY NA MKUU WA WILAYA YA UBUNGO​

Kumekuwa na taarifa inayosambaa kwenye mitandai ya kijamii kuhusu Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kumkamata mwandishi wa habari ambaye pia ni Mhariri wa biashara na Mkuu wa Kitengo cha Mtandao (digital) Ndugu Dickson Ng’hily kutoka gazeti la The Guardian.

Taarifa hiyo imeeleza pia mwandishi huyo alipigwa sana na kuumizwa kwenye mkono na simu yake kuvunjiwa kioo huku sababu ikielezwa kuwa ni kupiga picha wanafunzi wa shule ya msingi Kwembe waliokuwa wanasoma chini ya mti. Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa mwandishi hiyo alipelekwa ofisi ya Serikali ya Mtaa na baadaye kushikiliwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilya ya Ubungo.

Kupata mwanzo wa stori hii soma: Mwandishi wa Habari wa The Guardian anadai amepigwa na Walimu baada ya kupiga picha Wanafunzi wakisoma chini ya miti

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo anapenda kukanisha taarifa hiyo iliyoleta taharuki kwa wananchi na waandishi wa habari. Ukweli ni kwamba mwandishi huyo hakupingwa na mtu yeyote isipokuwa aliulizwa na Mwalimu Mkuu kwa nini anapiga picha bila ridhaa yao wala kujitambulisha.

Baada ya mwandishi huyo kukataa kutoa ushirikiano alipelekwa ofisi ya Serikali ya Mtaa na baadaye akapelekwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwaajili ya kujiridhisha kama kweli ni mwandishi na ana kibali cha kufanya kazi hiyo.

Kupata tamko la THRDC kukemea kitendo hicho soma: THRDC yakemea Mwandishi wa Habari kukamatwa kwa kupiga picha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwembe wakisoma chini ya mti

Hata hivyo leo Julai 10, 2024, Mhe. Mkuu wa Wilaya alikuwa kwenye ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani kwaajili ya kusikiliza kero za wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mburahati na hivyo hakuhusika wala kutoa amri yoyote kuhusu kukamatwa kwa mwandishi huyo.

Aidha, ni kweli kuwa wanafundi walikuwa nje ya madarasa yao kwaajili ya progeamu maalum ya kufanya masahihisho ya mitihani wa Utamilifu (mock) Mkoa, hivyo kimsingi shule haina wanafunzi wanaosomea nje kwa kukosa madarasa.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inathamini na kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari katika kufanikisha kazi yao muhimu ya kuhabarisha umma juu ya shughuli mbalimbali za maendeleo. Hata hivyo, ni muhimu waandishi wa habari kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo katika kutimiza haki yao ya kutafuta, kuchakata na kusambaza habari.

Signed
Joina Nzali

KAIMU MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

1720675451132.jpeg
===

Pia soma:
 
Ndugu nakupa hii chukua hakuna watu wana nguvu kama waandishi wa habari ,
Chukua tena tukio lolote likimuhusu mwanahabari serikali inahaha vibaya mnooo,
Nakuongezea hii, KALAMU ina nguvu kubwa kuliko unavyofikiria
Waandishi wa bongo vilaza chawa
Wana nguvu Gani?
Kabendera alipokamatwa waliofanya Nini?
 
Kajichanganya vipi na machangudoa ?Prostitution is a crime. Au kupambana na uhalifu sio kazi ya DC ?
 
Ndugu nakupa hii chukua hakuna watu wana nguvu kama waandishi wa habari ,
Chukua tena tukio lolote likimuhusu mwanahabari serikali inahaha vibaya mnooo,
Nakuongezea hii, KALAMU ina nguvu kubwa kuliko unavyofikiria
Tunawajua waandishi waliotikiswa kwa kesi ya kuhusisha serikali na kimya kimya mambo yao yaliisha, hawajatikisa serikali.
 
Kajichanganya vipi na machangudoa ?Prostitution is a crime. Au kupambana na uhalifu sio kazi ya DC ?
Tatizo ni kuthibitisha hiyo crime mahakamani. DC ni mshamba sana kudhani maDC wengine ni mafala kuwakalia kimya machangudoa.
 
Hana muda hapo mi nakuambia,
hana muda mrefu kivipi ?

hakuna mwenye muda mrefu kwa saab Samia anapenda teua tumbua kila asubuhi na jioni. Chalamila, Makonda, Makalla, Makamba, huyu dada kidoti, kawapachika pachua mara ngapi ? Mama Samia gets tickled doing reshuffles.

Nani alijua Zahra Yunus ataondolewa Ikulu that fast, given the pomp and pageantry za uteuzi wake kutoka Uingereza ?

DC wa Ubungo ataondoka kama ambavyo kila mteule wa Samia ataondoka within 6 months on average. Lakini sio kwa sababu kashindwa kazi. Prostitution is a prosecutable crime.
 
Tatizo ni kuthibitisha hiyo crime mahakamani. DC ni mshamba sana kudhani maDC wengine ni mafala kuwakalia kimya machangudoa.

DC wa ubungo hawezi kufanya kazi kwa kuangalia ma DC wengine wanafanyaje. This country is a failed state, a third world banana republic, viongozi wengi ni uozo, hawafanyi kazi zao. Tunataka viongozi ambao watajaribu kuwa tofauti. DC wangu wa huku crime infested Mbagala Rangi Tatu wala simjui, sijawahi kumsikia. DC wa Ubungo hawezi kumuiga mtu kama huyu!

Kuthibitisha crime mahakamani sio kazi ya DC. Kazi yake ni kumuagiza OCD aanzishe mchakato wa kisheria kwa kukamata!

Mabosi wa Polisi wa Ulaya wakisema tunakamata wahalifu prosecutor anawaachia, wananchi wana protest! Prosecutor anatimuliwa!

Utasemaje huwezi kuthibitisha jinai mahakamani ? Kwa nini ipo kwenye buku la makosa ya jinai?

We want more of the tough-on-crime, quality of life-minded district executives like Ubungo's Hassan Bomboko.
 
Back
Top Bottom