Serikali yakiri kuwepo uhaba wa vifaa tiba vya Saratani na Kisukari

Serikali yakiri kuwepo uhaba wa vifaa tiba vya Saratani na Kisukari

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema watu 25,000 walifariki kwa ugonjwa wa Saratani ndani ya mwaka 2020 pekee na kuufanya ugonjwa huo kuwa tishio zaidi ya Uviko-19 ilioua watu chini ya 1,000 hadi sasa.

Waziri Ummy pia amekiri kuwepo kwa uhaba wa vifaa tiba na dawa kwa wagonjwa wa Saratani na Kisukari na kueleza kuwa wanaoumwa magonjwa hayo wanakosa huduma kwa sababu ya gharama kubwa za dawa.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani, zinaonesha kwa nchi za Afrika, chini ya 30% ya Wagonjwa waliogunduliwa na Saratani wanaweza kupata matibabu, huku Saratani za Mapafu, Matiti, Utumbo Mdogo na Mkubwa na Saratani ya Mlango wa Kizazi zikiendelea kuwa tishio kwa nchi za Afrika.
 
Back
Top Bottom